Wakala wa Huduma za Ajira Tanzania (TaESA), kwa kushirikiana na Wakala wa Ufilisi na Udhamini (Rita), wamewatahadharisha wananchi kujiepusha na matapeli wanaowalaghai kutoa ajira mradi wa bomba la mafuta kutoka Uganda hadi Tanga.
Akizungumza na MCL Digital leo, Ofisa Habari TaESA, Jamila Mbarouk, amesema matapeli hao hutangaza kutoa fursa za ajira kupitia fomu zenye nembo za taasisi hiyo ya TaESA huku wakiwataka walipe hela. TaESA wamesema hawawatambui watu hao