Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Samuel Umtiti anayesakwa na Manchester United amefichua taarifa kuhusu utashi wake wa kubakia Barcelona. Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 24 anayecheza safu ya kati - nyuma anasema kuwa hataondoka klabu hiyo ya Uhispania labda afukuzwe. (Sun)
 
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho ana hofu juu ya ushindani wa malipo ya kifedha usajili wa mchezaji wa Wales Gareth Bale kutokana na bei yake, huku Real Madrid ikitarajiwa kumuuza mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28 kwa bei ya pauni milioni 200 (Express)
 
Liverpool wako tayari kujiandaa kusaini mkataba na nahodha wa timu ya Lyon Nabil Fekir huku mzungumzo kuhusu uwezekano wa kusaini mkataba wa pauni milioni 60 na mchezaji huyo wa safu ya kati mwenye umri wa miaka 24 yakitarajiwa kuanza wiki hii. (Goal)
 
Manchester City wamekataliwa kumnunua mchezaji wa kiungo cha kati wa Napoli Jorginho kwa pauni milioni. Klabu hiyo ya Ligi kuu ya Italia (Serie A ) wanataka walipwe pauni milioni 52 kwa mtaliano huyo mwenye umri wa miaka 26, na wanakabiliwa na ushindani kutoka upande wa Chelsea. (Mirror)
 
Juventus inaweza kumruhusu mshambuliaji Gonzalo Higuain kuondoka kwneye klabu hiyo, ikiwa watapata mkataba unaofaa msimu huu, huku Chelsea wakioongoza katika kutimiza vigezo vya kumchukua raia huyo wa Argentina mwenye umri wa miaka 30. (Calciomercato)
 
West Ham wako makini kwa mchezaji wa kiungo cha kati wa Fiorentina Milan Badelj. Badelj mwenye umri wa miaka 29 hana mkataba msimu huu, lakini klabu hiyo ya Italia inaamini atasaini mkataba mpya. (Tutto Mercato Web)
 
Mlinzi wa Atletico Madrid Sime Vrsaljko anasema anafurahia kuwa klabu hiyo ya Ligi ya Uhispania, licha ya taarifa kwamba Manchester United wanataka kusaini mkataba na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26, na mchezaji wa kimataifa wa Croatia. (Sportske Novosti - in Croatian)
 
Samuel Umtiti anayesakwa na Manchester United amefichua taarifa kuhusu utashi wake wa kubakia Barcelona. Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 24 anayecheza safu ya kati - nyuma anasema kuwa hataondoka klabu hiyo ya Uhispania labda afukuzwe. (Sun)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…