Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Takriban Watoto milioni moja wamezaliwa kutokana na watu waliokutana kupitia Match.com

Mtandao wa match.com unadai kuwa takriban watoto milioni moja wamezaliwa kutokana na watu waliokutana kwenye tovuti hiyo ya kutafuta wapenzi.
 
China ina kambi za kutibu waathirika wa kutawaliwa na mtandao (internet addict)

Wakati china ikiwa na watumiaji wa intaneti wapatao zaidi ya milioni 721, inaaminika kati yao milioni 23 ni waathirika wa kutawaliwa na mtandao. Hivyo wameanzisha kambi mbalimbali za kuwasaidia watu hawa.
 
Watumiaji wengi wa intaneti ni roboti na programu haribifu (malware)

Wakati mwingine unaweza kufikiri watumiaji wa mtandao ni watu pekee. Lakini asilimia kubwa ni roboti na programu haribifu zilizobuniwa na watu mbalimbali ili kutimiza shughuli fulani.
 
Huwa unatumia kisehemu kidogo tu cha mtandao

Ni wazi kuwa sehemu unayoitumia kwenye intaneti ni sehemu ndogo sana ambayo inaonekana kwenye injili pekuzi (search engines). Ipo sehemu nyingine ambayo imefichwa kwenye injini pekuzi (dark web); sehemu hii inajumuisha taarifa binafsi za watu, taasisi na makampuni mbalimbali.
 
IMDb ilikuwepo tangu miaka ya 1990

Tovuti maarufu ya kutafuta video, filamu, vipindi vya televisheni pamoja na michezo ya video ilianzishwa mnamo Oktoba 21, 1990, na Col Needham. Baada ya miaka minne ilipata jina lake la IMDb ambalo imedumu nalo hadi leo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…