Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Emery amesema kwamba anaamini wachezaji anaowataka ni wakali wenye vipaji vya hali ya juu na kwamba Arsenal inapaswa kunasa huduma zao ili kuja kufanya kweli kwenye Ligi Kuu England msimu ujao.

Ripoti za kutoka Hispania zinadai wachezaji wanaopendekezwa na kocha huyo Mhispaniola wasajiliwe huko Arsenal ni pamoja na winga wa Villarreal, Samu Castillejo, kiungo mkabaji wa Real Sociedad, Asier Illarramendi na beki wa kati wa Getafe, Djene Dakonam.
 
ACHANA na uvumi wa mitandaoni uliosambaa juzi kuhusu Arsene Wenger na Real Madrid.

Kocha hasa anayetakiwa na wababe hao wa Santiago Bernabeu baada ya kocha wake, Zinedine Zidane kuachia ngazi ni huyu hapa.

Mauricio Roberto Pochettino Trossero, kocha wa Tottenham ndiye chaguo la kwanza la Real Madrid katika mchakato wake wa kumpata kocha mpya wa kuchukua nafasi ya Zidane ambaye kuondoka kwake ghafla kumewashangaza wengi.
 
Zidane aliondoka juzi Alhamisi ikiwa ni siku tano tu baada ya kuipa ubingwa wa tatu mfululizo wa Ulaya Real Madrid kwa kuichapa Liverpool mabao 3-1 katika pambano la fainali lililopigwa jijini Kiev, Ukraine. Nafasi yake haikuwa hatarini.

Mfaransa huyo ambaye alikuwa staa mkubwa wa soka enzi zake alidai Real ilikuwa inahitaji ‘sauti mpya’ klabuni hapo ingawa alikanusha labda uamuzi wake umetokana na shinikizo la wachezaji wakubwa klabuni hapo.
 
Sasa vyanzo vya karibu vya Madrid vinadai Rais wa klabu hiyo, Florentino Perez anamtaka Pochettino ambaye ni Muargentina kwa ajili ya kukisuka upya kikosi cha Madrid lakini hata hivyo, bado klabu hiyo haijaongea na Pochettino mpaka sasa.

Pochettino alisaini mkataba mpya wa miaka mitano Tottenham mapema wiki iliyopita na habari za ndani zinadai hakuna kipengele kinachomruhusu kuondoka White Hart Lane kwa dau fulani la pesa.
 
Mwenyekiti wa Tottenham, Daniel Levy anajulikana kwa tabia yake ya kuwabania watu wake muhimu wasiondoke kikosini humo lakini hatakuwa na ubavu wa kumkatalia Pochettino asiondoke kama Real ikimfungia kazi ingawa inajulikana atataka kiasi kikubwa cha pesa kama fidia ya kuvunja mkataba wa kocha huyo.
 
Tottenham ilionyesha kiwango kikubwa katika mechi zake za Ligi ya Mabingwa wa Ulaya dhidi ya Real Madrid hatua ya makundi na mapema mwaka huu mchambuzi mahiri wa soka la Kihispaniola, Guillem Balague aliripoti Perez anamWona Pochettino kama kocha wa kuchukua nafasi ya Zidane akiondoka.
 
Wenger aliwahi kukataa hapo zamani lakini kwa sasa hayupo katika nafasi kabisa. Hamu ya Real Madrid kumnasa Pochettino ipo wazi. Ni aina ya kocha ambaye Real Madrid ingependa kuwa naye wakati fulani,” alisema Balague.
 
Hata hivyo, tamaa ya kurudi Hispania ambako aliwahi kufundisha klabu ya Espanyol kuanzia mwaka 2009 hadi 2012 kabla ya kwenda Southampton inaweza kuwa kubwa na itakuwa vigumu kwake kukataa fursa ya kufundisha timu kama Real Madrid.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…