Wewe unajua una ndoa yako, unachepuka hadi unazaa nje ya ndoa kisha unawakana watoto wako, hutoi matunzo, hali hii inasababisha watoto kukosa haki ya msingi ya chakula, afya na elimu na kusababaisha ongezeko la watoto wa mtaani au Panya Road.
“Baada ya mahakama kukutia hatiani, ili iwe fundisho kwa wanaume wengine wenye tabia kama hizi, mahakama inakupa adhabu mbili.
“Kwanza utatumikia kifungo cha miezi mitatu jela. Pili utalipa faini ya shilingi laki tano na mwisho ukimaliza adhabu hizo, utawajibika kuwatunza watoto hawa mpaka watakapojitegemea,’’ Hakimu Mwambusi alimweleza Hamis wakati akimsomea hukumu hiyo.
Baadhi ya watu waliofurika mahakamani hapo kufuatilia kesi hiyo waliipongeza mahakama kwa kutoa adhabu hiyo.