Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

naweza kufikiri tofauti kidogo kutokana na wasomi na wengine wanavyofikiria siku hizi , tunaweza kubishana kuwa maisha hayana maana halisi , tupo tu kwa ajili ya kuzaa ili tuongezeke. Lakini hii sio maana halisi ya maisha.
 
Tunaweza kusema kuwa na dini fulani ili ufike mbinguni, maisha ni kujulikana, ni kujaribu kuifanya Dunia kuwa mahali pazuri pa kuishi, lakini yote tunayofanya tunafuata mambo yale yale yaliopita zamani , mipango iliyopita, hata ufahamu wetu tulionao tunafikiri tuna uzoefu wa kitu fulani ndani ya vichwa vyetu ambavyo havijawahi kutokea, au vinatokea tu kama kivuli kwenye kazi za ubongo wetu. Ni kweli ndani yetu tuna vitu vikubwa lakini hatuelewi.
 
Mimi nafikiri ipo maana ya maisha lakini bado hatujaelewa, tunajiona kama tumetengenezwa na mashine au tunaishi kwa kutegemea mashine iliopo ndani yetu. Sidhani kabisa kama maisha hayana maana kati ya kuzaliwa na kufa kuna kitu mtu anatakiwa kukifanya ili aweze kufurahia maisha yake ya huo muda. Na hii sio kwa sababu mimi ni mtu wa dini sana hapana .
 
Kwa hio kwa nini nafikiri maisha yana maana ? huenda nimekuwa disappointingly, Ni ngumu kuweka katika maneno, lakini ngoja nijaribu japo kidogo.

Mateso ya mwanadamu Huletwa na Mabadiliko Ya Uzoefu

Katika miaka 10 ya uzoefu wangu nimeona watu ambao hupitia mateso hukutana na matatizo makubwa hasa maradhi ya saratani na kisukari na hata ugonjwa mbaya wa moyo na kusababisha vifo vya haraka.
 
Kitu gani hasa kinawapata hawa watu , ni kwa sababu kila wanapoamka hawachukui maisha mazuri yanayoachiliwa na Mungu kwa sababu ya kuzoea mateso, hawana ufahamu wa kutosha kuhusu maisha, wanamiliki miili badala ya Roho, wameshindwa kujiunganisha na watu wazuri, ni watu wanaoweka mioyo yao kwenye vitu sio kwa Mungu. Wanasahau vitu vya muhimu kama Upendo , Amani, Furaha, Fadhili Uaminifu na mengine. Wanakimbizana na vitu. Kutafuta Pesa Ili kujilinganisha na wengine.
 
Baadhi Ya mifano

Kuna mama mmoja ambaye alikuwa amepimwa na kuonekana na saratani alisema hivi, Nashukuru Mungu kuwepo kwenye sayari hii.. Nahisi ni bahati ya ajabu kwepo na kuweza kupata ufahamu huu . Mtu mmoja aliniambia kuwa nikitumia pombe nitajisikia vizuri na kuwa mwenye nguvu, pia nitajiona kuwa salama, nitajitambua na kugundua siri za ajabu katika Dunia hii.
 
Mtu mwingine anasema kwamba anasikitika kwa kuwa amepoteza muda mwingi kutokubaliana na vitu vidogo , yeye alikuwa anataka kupata vitu vikubwa kwa mara moja ili kukamilisha malengo yake kwa upesi zaidi, akawa anahitaji pesa nyingi na kwa kuwa hakuwa na ufahamu , hakuwa na maarifa wala Ndani yake hapakuwepo hekima ya Mungu . alikuwa gizani kwa kiasi kikubwa , Sasa anateseka . hakujua kabisa maana ya maisha . Ingawa baadae aliona maana ya maisha ni kujifunza sio kutafuta pesa, kukua na kupata uzoefu kwanza.
 
Hawa watu wote hawakuwahi kusikia kuokoka , hawakuwa watu wa kujifunza , walikuwa wanawaza pesa ili kununua vitu nao waonekane . Ipo njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu, lakini mwisho wake ni njia za Mauti.
 
Haya mabadiliko hayawezi kuja kwa haraka yanachukuwa muda mrefu. mpaka mtu afundishwe afahamu ndio atagundua maisha ni nini. Nafikiri mabadiliko yanaweza kuelezewa kwa namna nyingi ili kuleta maana halisi ya maisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…