Maisha yanapaswa kufurahiwa. Lakini kama hufurahii kazi yako, lazima ikuchoshe kufanya kazi mchana kutwa. Kila mtu lazima ana hobby anayoifurahia. Ni njia ya kujionesha mwenyewe na kujisikia vizuri. Kinachofurahisha zaidi ni kuwa wakati mwingine unaweza kuifanya hobby yako ikulipe.
Baadhi ya hobby kama vile kucheza vvyombo vya muziki au ujuzi mwingine, ni nzuri kuwahusisha watu. Kumfundisha mtu kucheza chombo cha muziki au kutengeneza kitu kunaweza kulipa. Toa mafunzo mara kwa mara, kila wiki au kila mwezi au toa semina kwa watu wenye hobby kama yako lakini wanaopenda kujua zaidi.
Tafuta kazi unayoendana nayo
Baadhi ya hobby ni ngumu kuzigeuza kuwa biashara. Jaribu kuangalia kazi ambazo zinaendana na hobby yako. Unapenda maua? Kuwa mtu wa bustani. Unapenda kufanya mazoezi? Kuwa trainer. Unaweza usipate kile kile unachotaka, lakini ukipata kazi ambayo unaweza kushare maarifa kwenye suala Fulani ni kitu cha kizuri.
Weka online
Labda hupendi kuuza ama kufundisha. Blog kuhusu kitu hicho. Tengeneza website yako mwenyewe na share passion yako kwa wengine. Chukua picha na onesha ubunifu. Kadri watu watakavyoipata website yako, ndio utapata faida zaidi hasa kama unataka kupata matangazo. Ongea kuhusu mada kuvutia, share mambo yako, ni website yako kwahiyo fanya upendacho.
Hitaji lako la kwanza ambalo unatakiwa ulijue katika safari yako ya mafanikio ni kwamba, unahitaji sana kujifunza, kukua na kuendelea kufanikiwa yaani learn, grow and develop. Hilo ndilo hitaji lako la kwanza.
Kila wakati utahitaji ujue ni nini ufanye ili kuboresha maisha yako au ufanye nini cha zaidi ili hicho unachokifanya kikuletee matokeo makubwa na unayoyataka kwenye maisha yako leo na hata kesho.
Unaweza ukaanza kuboresha chochote kile hata kwa kidogo sana. Unaweza ukaanza kuboresha tabia zako, unaweza ukaanza kuboresha biashara yako au hata maarifa yako kwa kujisomea zaidi na zaidi kila siku.
Kuendelea kujitoa kikamilifu na kuboresha maisha yako linatakiwa liwe zoezi endelevu, kila siku jiulize, ni kwa namna gani unaweza ukafanya siku yako ikawa bora, ni namna gani unaweza kuboresha maisha yako kuliko jana?
Kufanya mabadiliko na kubadilisha maisha yako, ni jambo ambalo linachukua muda( Becoming a master takes time). Unatakiwa kujifunza na kuchukua mazoezi tena na tena ili kuwa mbobezi. Hakuna kikubwa ambacho utakachofanikisha kama usipofanya hivyo.
Hakuna mpaka wa kuboresha maisha yako, hakuna mpaka unaokuzuia wewe kukua kimafanikio. Kila iitwapo leo, endelea kuboresha maisha yako kwa jinsi unavyoweza. Ukiendelea kufanya hivyo, uwe na uhakika utafanikiwa.
Jiulize kipi kinachokuzuia ili usifanye maisha yako yawe bora? Angalia usikwamishwe na hofu wala usikwamishwe na tabia za kuahirisha mambo kila wakati. amua kufanya kitu kitakachoyafanya maisha yako yaonekane ya maana.
Kama nilivyosema mwanzoni mwa makala haya, unahitaji sana kujifunza, kukua na kuendelea kufanikiwa. Kila siku jiulize, je, umejifunza nini? Je, kutokana na kujifunza huko kuna hatua yoyote unayopiga?
Kama hujifunzi elewa hautaweza kukua, wala hautaweza kufanikiwa. Maisha ya mafanikio ndivyo yapo hivyo, yanahitajji kuweka juhudi nyingi katika .katika kila eneo ili uweze kupiga hatua za kimafanikio.