Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

ENGLAND bana, kweli wana kiherehere. Kombe la Dunia linaanza wiki ijayo huko, lakini wao tayari wameshaweka hadharani kikosi chao kitakachoanza kwenye mechi ya kwanza na Marcus Rashford ataanzia benchi licha ya kuonyesha kiwango kikubwa kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Costa Rica, Alhamisi iliyopita
 
Kocha Southgate amesema ameamua kumwanzisha Rose baada ya kukoshwa na kiwango chake katika mechi zilizopita licha ya staa huyo wa Tottenham Hotspur kutokea kwenye maumivu makali ya goti miezi 16 iliyopita. Kikosi hicho kilivyo, mabeki wa kati watatu ni Harry Maguire, John Stones na Kyle Walker, huku wachezaji wengine walioanza kikosini ni Trippier, Jesse Lingard na Dele Alli.
 
HUKO Russia kwenye Fainali za Kombe la Dunia kutakuwa na wanasoka 736 watakaopigana vikumbo kuunasa ubingwa huo wa dunia.

Lakini, wachezaji hao kila mmoja ana sifa yake na hakika hicho ndicho kitu kinachowavutia zaidi mashabiki kutaka kufahamu kuna mastaa wa aina gani watakaokuwapo kwenye mikikimikiki hiyo.
 
HUKO Russia kwenye Fainali za Kombe la Dunia kutakuwa na wanasoka 736 watakaopigana vikumbo kuunasa ubingwa huo wa dunia.

Lakini, wachezaji hao kila mmoja ana sifa yake na hakika hicho ndicho kitu kinachowavutia zaidi mashabiki kutaka kufahamu kuna mastaa wa aina gani watakaokuwapo kwenye mikikimikiki hiyo.
 
Nchi zinazoshiriki ni 32 na kila moja imejumuisha wachezaji 23 kwenye kikosi chake, lakini sasa unamfahamu mchezaji mfupi kuliko wote, mchezaji mwenye kilo nyingi, au mchezaji mwenye uzito wa unyoya au yule mdogo zaidi na mkubwa zaidi?
 
Mchezaji mwenye kilo nyingi

Staa wa Panama, Roman Torres, ndiye mchezaji mwenye kilo nyingi zaidi kati ya wale wote waliopo kwenye fainali za Kombe la Dunia huko Russia. Staa huyo ana uzito wa kilogramu 99. Torres ni beki, hivyo kwa washambuliaji wenye kilo za kuku wajipange kabisa kwenda kukutaka na mtu mzito. Bao lake dhidi ya Costa Rica ndilo lililoipa Panama tiketi ya Kombe la Dunia huko Russia.
 
Mchezaji mwenye kilo chache

Japan hakika ndiyo timu yenye wachezaji wengi wenye uzito mdogo na hapo, kiungo wao wa ushambuliaji, Takashi Inui, ndiye mchezaji mwepesi zaidi kwenye fainali hizo za Russia, akiwa na kilogramu 59 tu. Amejiunga hivi karibuni huko Real Betis akitokea Eibar na ameichezea timu yake ya taifa mara 21. Wachezaji wenyine wenye uzito wa unyoya kwenye fainali hizo ni Jesse Lingard (England) kilo 60, Joao Moutinho (Ureno), Al-Breik Mohammed (Saudi Arabia), Nahitan Nandez, Lucas Torreria (Uruguay) na Dries Mertens (Ubelgiji) ambao kila mmoja ana kilogramu 61.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…