Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Hii itakuwa ni shughuli kati ya bara Ulaya inayojidai kuwa na soka bora duniani, dhidi ya Waasia wabishi kutoka Japan. Itakuwa ni hadithi ya mende kujaribu kuangusha kabati. Sina haja ya kufafanua maana sote tunajua mende ni nani na kabati hapo ni nani!
 
Ubelgiji inajivunia kuwa nyota kibao, wanaosakata soka katika klabu kubwa huko Ulaya. Yupo Romelu Lukaku, Eden Hazard, Maroune Fellaini na Thibaut Coutouis. Wajapani wanae Shinji Kagawa na Keisuke Honda. Majina mengine ni magumu sana, nisije vunjika ulimi bure
 
Wawili hawa watakutana katika mchezo wa sita ya hatua ya 16 bora, utakaopigwa kesho, katika uwanja wa Rostov Arena, mjini Rostov, yapata kilomita 215.2 kutoka Moscow, kuanzia saa tatu usiku, mara baada ya kumalizika kwa vita ya Amerika kusini dhidi ya Kaskazini (Brazil v Mexico).
 
Baada ya kuipiga Three Lions na kuchukua uongozi wa kundi G, Belgium walikata tiketi ya kwenda Rostov, kuwakabili Samurai Blue, wakiwa na matumaini ya kuwafuata Uruguay na France, waliotangulia robo fainali.
 
Vijana wa Roberto Martinez wanaingia katika mchezo wa kesho wakiwa na morali hii ni baada ya kuitandika Japan, iliyokuwa chini ya Vahid Halilhodzic, (Akira Nishino ndio kocha wa sasa), bao 1-0 katika mechi ya kirafiki miezi chache iliyopita (Novemba 2017). Wanajiamini kinoma.
 
Kama ulifikiria ni ndoto kwa mende kuangusha kabati, fahamu kuwa Mashetani wekundu wamefanikiwa kuifunga Samurai Blue mara moja tu katika mechi tano walizokutana hivi karibuni. Wameshinda moja, sare mbili wakachapwa mara mbili. Umeshanisoma?
 
Kama ulifikiria ni ndoto kwa mende kuangusha kabati, fahamu kuwa Mashetani wekundu wamefanikiwa kuifunga Samurai Blue mara moja tu katika mechi tano walizokutana hivi karibuni. Wameshinda moja, sare mbili wakachapwa mara mbili. Umeshanisoma?
 
Kitakwimu Belgium ni watoto tu kwa wajapani hawa. Hata hivyo, hii haimanishi kuwa Japan wameshafuzu, kutakuwa na shughuli sio kidogo, kwa sababu, Belgium mpaka sasa ndio timu iliyofunga mabao mengi (9). Pia ni moja kati ya timu zilizoshinda mechi zao zote tatu za makundi, pamoja na Uruguay na Croatia.
 
Sio kwamba nawatisha wajapani lakini, Belgium hii hii, inajivunia kucheza mechi 22 bila kufungwa. Wameshinda mara 17 na sare tano. Mara ya mwisho kufungwa ilikuwa ni Septemba, mwaka 2016, ambapo walichapwa 2-0 na Spain.
 
Kama hiyo haitoshi kuonesha ugumu wa mechi ya kesho, chukua hii, Romelu Lukaku amefunga mabao 23 katika mechi 20 alizoingia dimbani kuichezea Belgium chini ya uongozi wa Roberto Martinez na benchi lake la ufundi linaloundwa na wanaume kama Thiery Henry.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…