Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

LAKINI pia inawezekana wewe ni mmoja kati ya hao ambao wana sononeko la MOYO kwa kutopata faraja ya kweli kwa WAPENZI wao .
lakini hpa nina zungumia kutopata mpenzi kwa muda mrefu,na sasa umekata tamaa ya kupendwa,kuolewa/kuowa katika siku zote za maisha yako .lakini labda wakati mwingine inawezekana hujafahamu chanzo cha wewe kutopata MPENZI .. Kumbuka kuna mambo mengi ya kuzingatia ili uweze kupata MTU ambaye atakuwa mume/mke yaani mwenye MAPENZI ya kweli nawe.
 
JE..? UNAJIJALI..hapa unaweza ukajiuliza maswali mengi kutokana na nilivyouliza je unajijali!, hapa nina maanisha je unajipenda?, kwani unadhani kama wewe hujijali ,hujidhamini, nani atakupenda? unatakiwa ujipende kikawaida wewe mweyewe kabla ya kuhitaji upendo wa mtu mwingine, inawezekana hujitunzi,unjiweka hovyohovyo, hivi fikiri ni nani atakupeda katika misingi hiyo..,Lakini sina maana ya wakati wote uwe smart,kwani kwa kuwa inawezekana wenginine wanafanya kazi ngumu ambazo mazingira yake hayaruhusu,lakini baada ya kazi unaoaswa kuwa msafi mbele za watu.
 
Kwa upande wa wasichana sio lazima uweke nywele zako dawa au usuke rasta wakati vitu hivyo huna uwezo navyo,wakati kumbe unaweza kusuka nywele zako vizuri au wakati mwingine ukanyoa mtindo mzuri unaokubalika katika jamii huku ukijistiri kwa ushungi kichwani mwako. Anza kujipenda kabla ya kuhitaji upendo kutoka kwa mtu mwingine.
 
JE UNAJIAMINI..? kutokujiamini pia hili ndio tatizo ambalo ni la kisaikolojia zaidi,kwa sababu kuna baadhi ya watu wanakosa kujiamini, hii hupelekea mtu mwingini kuamuakukaa kwenye kioo na kuanza kujikosoa yeye mwenyewe,kwa kujitoa kasoro mbalimbali katika mwili wako na umbile lake jinsi alivyoumbwa na mola wake,hujiona mbaya,havutii,na mbaya zaidi kujiona yeye hana hadhi katika ulimwengu wa mapenzi.
Nani amekwambia eti una kasoro,,uachotakiwa ni kmshukuru mwenyezimungu kwa kukuumba jinsi ulivyo. Amini kuwa mungu ana makusudio yake kukuumba jinsi ulivyo.kwani kuna watu wengine wanaweza kukupenda kutokana na hizo kasoro unazoziona katika mwili wako.
 
Kujitoa kasoro,kutojiamini ni kosa kwa kuwa unajiathiri kisaikolojia na kujiona hufai kupendwa. na mwisho wa yote unakuja kumparamia mtu yeyote kwa lengo la kujiondolea mkosi! na akishakukutumia anakuacha solemba unabaki na machungu moyoni na kujiongezea matatizo zaidi.
 
Naamini baada ya kujipenda wewe na KUJIAMINI kuwa hauna kasoro na unavutia, basi utakuwa na hali ya kawaida kisaikolojia na wakati mwingine anaweza akajitokeza akupendaye na akakuomba hifadhi ya moyo wako kwake.
 
Sababu ya kukaa muda mrefu bila MPENZI au kutamkiwa kuwa unapendwa isiwe chanzo cha kupata maumivu mapya ya moyo. Acha papara,Tulia,Pata wasaa wa kumchunguza huyo anaedai anakupenda kwa muda wa kutosha kwa kuwa inawezekana naye akawa ni mmoja kati ya wale wanaotaka kukufanya kama chombo cha Starehe tu..!
 
Kwa dada zang baada ya Mwanaume kukuomba uwe nayw pamoja unatakiwa pia umchunguze kwanza na usiruhusu aujue mwili wako kabla ya kuelewa nia yake hasa kwako ni ipi..Starehe ya muda mfupi au anakuhitaji kimaisha{NDOA]. Hivyo basi usifanye mambo kwa papara,hitaji utulivu wa kutosha ili uweze kupata yule ambae ni muhimu kwa ajili yako.
Ukijiamini na Kuwa makini ni wazi kuwa utampata yule anae kupenda kwa dhati...
 
Maneno 25000,,ase kuna wanawake wanaongea km cherehani vle,, anawakia kwnye Gear
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…