Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Tamaa mbaya ni hali ya kutaka kumiliki mali zaidi ya mahitaji halisi; hali ya mtu kutotaka kuridhika, kwa mfano, kurudia rudia chakula ili hali watu wengine wanakosa. Tasnia ya matangazo hutumia mwanya huu kwa kutoa matangazo bora yanayoteka akili za watu na kuwaamuru watu wagombanie bidhaa ili wapate furaha, kwa lengo la kuvutia wateja.
 
Kuingia kwenye madeni. Kutaka kujilimbikizia mali kunawafanya watu kukopa kwa pupa na kulipia mambo yasiyo na tija ya kweli kwao. Madeni hayo hupelekea mtu kudhalilika na kufilisiwa baada ya kushindwa kulipa.
 
Kuingia kwenye madeni. Kutaka kujilimbikizia mali kunawafanya watu kukopa kwa pupa na kulipia mambo yasiyo na tija ya kweli kwao. Madeni hayo hupelekea mtu kudhalilika na kufilisiwa baada ya kushindwa kulipa.
 
Kuvunja mahusiano ya mtu. Tamaa mbaya huleta mtafaruku hususani pale mtu anapoingilia na kuhatarisha maslahi ya mwenzie au jamii yake. Kwa mfano kusogeza mpaka wa shamba au kiwanja.
 
UKuleta tabia hatarishi. Tamaa mbaya hupelekea tabia hatarishi kama kukosa usingizi, kukosa hamu ya kula, hasira n.k. Hali hizo hupelekea kupungua kwa kinga ya mwili na uzito na hatimaye magonjwa​
 
Jinsi ya Kukwepa Tamaa Mbaya

1. kukubali mafanikio. Mtu anapaswa kutizama ubora wa mali alizo nazo, ikilinganishwa na awali, bila ya kuangalia nani anamiliki nini. Kuridhia mafanikio ni silaha muhimu sana.
 
Kujitathimini na kuweka malengo. Mtu anapaswa kujiweka mbali na hisia mbaya; hisia za kukosa, na kujiangalia kwa kina mahitaji halisi. Mahitaji halisi huwekwa kulingana na uwezo wa mtu husika.
 
Kukwepa kujithaminisha na mtu.
Mtu asifadhaike kutokana na hatua za mafanikio jamaa zake walizopiga, kwani kila mtu anapata fursa tofauti tofauti na kwa nyakati tofauti. Pia kamwe mafanikio hayawezi kufanana, kwani mafanikioa ni kama vidole.
 
Kuwasaidia wengine. Kuwawazia na kuwasaidia watu wanaokosa mahitaji ya msingi kama chakula, makazi na mavazi husaidia kupunguza tamaa mbaya kwa kiasi kikubwa, hii ni ngumu sana kwa watu wenye wivu. Ni muhimu kuwasaidia yatima, wajane, wazee wasio na walezi, vilema n.k.
Katika shida na tamaabu zao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…