"Ni muhimu kuhifadhi ndizi hizo za porini kwa sababu zina mbegu kubwa ambazo zinaweza kutoa fursa ya kutafuta jeni ya kuimarisha ndizi inayopandwa'', alisema.
Ndizi hiyo hukuwa kandokando ya pori ambapo ni rahisi kuharibiwa na hali mnbaya ya anga ,ukataji wa miti , moto, mbali na kukata pori kwa lengo la upanzi.
Ndizi zinatoka katika eneo moja ikimaanisha kwamba zote ziko sawa. Hivyobasi iwapo ugonjwa umepatikana katika mmea mmoja unaweza kuenea kwa kasi katika mimea yote.
Inapatikana katika pori la misitu ya kitropiki katika eneo la magharibi la taifa hilo ambapo inakabiliwa na hatari ya kukatwa kwa miti: Ni miti mitano pekee inayodaiwa kusalia katika pori hilo.