Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23], pepo?? Sio kweli hata kidogo...

Kwotesheni zisiwe nyingi tuokoe muda...
 
. Taarifa kutoka nchini Russia, zinasema kuwa, Shirikisho la soka duniani, FIFA, limeanzisha uchunguzi dhidi ya beki wa Croatia, Domagoj Vida, kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kutoa kauli za kibaguzi dhidi ya wachezaji wa Urusi, baada ya mechi iliyokutanisha timu hizo jana.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi kutoka makao makuu ya FIFA, ni kwamba shirikisho hilo, linachunguza madai kuwa beki huyo anayekipiga katika klabu ya Besiktas ya Ureno, alitoa matamshi yaliyotafsiriwa kuwa ya kibaguzi dhidi ya wachezaji wa Urusi, baada ya kumalizika kwa mchezo.
 
Russia na Croatia, ziliumana katika mchezo wa mwisho wa robo fainali, uliopigwa katika uwanja wa Fisht huko Sochi na Croatia wakaibuka washindi wa 4-3 kwa mikwaju ya penalti, kufuatia sare ya 2-2 katika dakika 120 ambapo Vida aliifungia Croatia bao la pili, kabla Hernandez hajaisawazishia Russia kunako dakika ya 115.

Kupitia mtandao wa kijamii, kwa njia ya video, Vida akiwa sambamba na nyota wa zamani wa Croatia, Ognjen Vukojevic, alisikika akisema: "Hongera kwa Ukraine." Unaweza ukadhani ni kauli ya kawaida kumbe kwa Warusi, ni kauli ya kibaguzi na ya uchochezi. Kwanini?
 
Kauli hii, imekuwa ikitumiwa na baadhi ya watu wa Ukraine, ambao ni wapinzani wakubwa wa Russia. Naye Vukojevic aliongeza: "Ushindi huu ni kwa ajili ya Dynamo na Ukraine"

Kama itathibitika kuwa kauli ilikuwa inalenga kuwaudhi Warusi hasa baada ya kubanduliwa mashindanoni, huenda Vida akashukiwa na rungu la adhabu kutoka FIFA, hii ni kwa mujibu ya kamati ya nidhamu ya shirikisho hilo.
 
FIFA inafuatilia baadhi ya ripoti za mechi ile ikiwemo swala hill, kama tutaridhika kuwa mchezaji huyu alifanya kitendo kile kwa kusudia kuwadhihaki Warusi, adhabu yake ni kukosa mechi mbili au faini, ieleweke kuwa vitendo vya kichochezi hasa vya kisiasa havirusiwi katika soka," ilisema taarifa ya FIFA.

Itakumbukwa kuwa mapema katika michuano hii, wachezaji wawili wa Switzerland, Granit Xhaka na Xherdan Shaqiri walipigwa faini baada ya kuonesha ishara ya ndege Tai ambayo ipo kwenye bendera ya Albania wakiimaanisha kuiunga mkono nchini ambayo ni taifa lao la asili, katika mechi dhidi ya Serbia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…