Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Zahanati yateketea kwa moto, watano wadakwa akiwemo mtendaji




Watu watano akiwamo ofisa mtendaji wa kijiji cha Ulaya, wilayani Igunga mkoani Tabora, Zablon Hussin wanashikiliwa polisi kwa mahojiano wakihusishwa na tukio la jengo la zahanati ya kijiji hicho kuungua moto.
 
Jengo hilo liliungua moto usiku wa Julai 14, 2018 na kusababisha hasara ya zaidi ya Sh85 milioni.

Akizungumza na wanahabari leo Jumamosi Julai 21, 2018 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Emmanuel Nley amesema majina ya watuhumiwa wengine wanaoshikiliwa yanahifadhiwa kuepuka kuharibu upelelezi.
 
Kaimu Mganga Mkuu wilaya ya Igunga, Dk Bonaventura Kalumbete amesema moto huo pia umeteketeza dawa na vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi ya Sh25 milioni.

Dk Kalumbete amesema juhudi zinaendelea kutafuta jengo jingine ili litumike kwa ajili ya huduma wakati mchakato wa ukarabati zahanati iliyoungua ukiendelea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…