Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

gerry.jpg
 
[HASHTAG]#inawezekana[/HASHTAG]
Ukiamini sana na kuvutiwa na uzuri wa ndoto unayotaka kuitimiza hutawaza sana juu ya adha za sori ya kiatu kuisha kwa kutembea huku na kule kukamilisha mchakato wa kutimia kwa ndoto hiyo. Wala hutakubaliana na watu wanaokwambia kwamba haiwezekani lakini na utapambana siku zote bila kuchoka.

Kumbuka kwamba katika mchakato wa kutimiza lile lililo moyoni mwako kuna mambo mengi madogo madogo ya kukatisha tamaa ambayo sio agenda kuu ya kuishi kwako usiyatazame hayo bali litazame lile unalotaka kulitimiza maana hilo likitimia litatatua matatizo unayoyaona ni issue sana mfano unaacha kutafuta wateja kisa unalinda sori ya kiatu chako kizuri, kisa unaogopa kuonekana hujala mchana maana midomo imekauka, kisa unaogopa kuonekana mjini na shati lile lile (kauka nikuvae ) wiki ya tatu sasa, kisa unaogopa kuonekana kwenye magari ya gongo la mboto posta mwaka wa pili sasa.

Hahaa watu hawatukuwa na muda na shati lako wala viatu vyako kama ukiwapa fursa ya kusoma mawazo yako. Usikate tamaa hata kama wengi wamekataa endelea kutafuta maana kuna watu wapo mahali fulani ambapo hujafika bado na hazina iliyo katika uwezo wa ufahamu wako ndio bidhaa adimu wanayotafuta na si shati au viatu ambavyo kwa sasa huna na mtu yeyote anaweza kuvipata kariakoo au makoroboi kwa wale ndugu zangu wa mwanza.

Usijiangalie nje sana ukahisi kujihurumia, kujidharau na kujizuia lakini angalia hazina uliyonayo na ni wangapin wanakuhitaji
 
Back
Top Bottom