Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Tabia bora ya afya ya akili.

1.Panga mawazo yako mwenyewe. Soma vitabu mbalimbali, sikiliza masomo yanayofaa kwenye akili yako. Achana na habari zinazokushambulia akili yako. Uwe na mtazamo ulio wazi, jaribu kusaidia wengine kama unaweza. Pata marafiki wapya, Jifunze njia mpya za mafanikio. Fikiria hekima ambayo unaweza kuijenga ndani ya miaka mitano na zaidi, kama utakuwa mtu wa kuuliza maswali na kutaka kujua.
 
2.Kaa mahali penye ukimya kwa dakika kadhaa kila siku. Hatuiti hii kama meditation, kwa sababu hapa hutaweza kunielewa. ni muda wa kutulia tu peke yako. Hauhitaji kukunja miguu, huhitaji kufunika macho. Ubongo wako unatakiwa kutulia. lakini usiongee wala kufanya kitu kingine, just sit, vizuri,na pumua kwa urahisi kwa muda wa dakika kadhaa.
 
3.Chukua karatasi na kalamu andika yaliopo akilini mwako, kisha yafute kabla hujaenda kulala . kwa sababu kufanya hivyo utapunguza au kuondoa kabisa wasiwasi na huzuni iliokuwepo ndani yako.
 
4.Jaribu kurudisha mawazo mazuri ili kuondoa stress iliokuwepo. Fanya kitu rahisi ambacho ni cha kukumbuka . Hii ni njia nzuri ya kufundisha ubongo wako. Na kusema kuwa kila kitu kitakwenda vizuri. Mimi napenda kusema hivi. Hata hili litapita tu. Nina nguvu kuliko ninavyofikiri. naweza kujifunza kila ninapohitaji kujifunza.Siko peke yangu. Kuna uhuru ndani yangu.
 
Tabia bora ya Mahusiano.

1.Piga simu, tuma ujumbe au email kwa familia yako au rafiki yako kwa siku. Hali hii mara nyingi inakuwa ni ngumu. Upo urahisi tu tunapokutana na wafanyakazi wenzetu tukiwa kazini, kwa sababu tunawaona kila siku. Fanya zaidi , katika kuwakumbuka familia, marafiki unaowathamini. Itakuchukua muda mfupi tu kufanya hivyo, Kuwa ni mawasiliano mazuri na watu wanaokuzunguka, wote wa karibu na wa mbali.
 
2.Waambie kuwa una shukuru kwa kuwa na familia hio, marafiki hao, Waambie maneno mazuri ya upendo, au andika kinote na ukitume , Ni vizuri kuwa mtu wa shukurani kuliko kuwa mtu mwenye woga. Jijenga katika kushukuru kwa kila kitu kilichopo maishani mwako.

Maliza siku yako kwa shukurani. Shukuru kwa ajili ya mwenza wako, masomo yako, kazi yako, watoto wako, maisha yako . hii inasaidia kuondoa mawazo mabaya na huzuni yeyote.
 
3.Jifunze kusikiliza badala ya kujibu. kwa kupata muda zaidi wa kufikiria wakati mtu mwingine anaongea. Hii sio tu inaonyesha kuthamini kile kinachoongelewa , ila inaonyesha kuheshimu na kukubali,pia inakupa muda wa kupima tabia na maneno.

Jipe muda wako mwenyewe, maisha yanatokea. utakapokutana na stress, kuchanganyikiwa , hasira, au kutovumilia wakati unapokutana na mambo mengi. Kama utakuwa na muda wako, utaweza kuweka mambo sawa, hutaendeshwa kama robot.
 
Jiambie maneno mazuri kila siku, maneno ya kukutia moyo, maneno ya kukujenga, maneno ya ujasiri, maneno ambayo yatakufanya uwaze mazuri .Jifanyie wema . Unachotaka kufanyiwa wewe, anza kujizoesha kuwafanyia wengine.
 
Jifunze kumkaribia Mungu ndani yako.

Toa maoni yako. Ngoja nikufundishe kitu kidogo hapa ninapokuambia toa maoni yako. ukipata kitu toa kitu. unapotoa maoni yako yanayohusiana na makala hii utawasaidia wengi. utakuwa umefanya kazi ya Kuelimisha kupitia hapa. Mungu akubariki unapofanya hivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…