Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

*ZAWADI KWENU WADADA*

*Wanawake Tambueni hili.*


Hakuna mwanaume mkorofi kwa mwanamke mnyenyekevu hata ungekua umemkosea nini ukijishusha ukanyenyekea analainika labda awe na hayuko Sawa ndio unyenyekevu wako hautagusa moyo wake....

Mume hafokewi, mume hagombezwi, mume humfanyii jeuri na kiburi, akinuna na wewe unanuna asipokutafuta na wewe humtafuti, utapoteza ndoa yako. Usiige maisha ya waliokosa adabu na malezi bora.

Ni mume wako wa ndoa unaruhusiwa kumng'ang'ania kama ruba. Asipokutafuta mtafute, asipoongea na wewe ongea naye wewe. Usisikilize maneno ya watu Kuwa mke akifanya hayo anajipendekeza kwa mumewe. Hayo ni maneno ya wakosaji. Haya na iwe unajipendekeza. Usipojipendekeza kwa mume ukajipendekeze kwa Nani?

Kunyenyekea hakukugeuzi housegirl na ukapoteza nafasi yako ya kuwa mke, ila kiburi na jeuri ndio vitakufukuza kwenye hicho kiti na hiyo nafasi ya kuwa mke haraka sana. Na kuchukuliwa na wengine kwa haraka zaidi ya sana.

Wako mamilioni wanaitaka nafasi hiyo. Tena warembo, wenye hadhi, wazuri na wenye Mali kuliko wewe. Ukimuona wa nini wenzako wanajiuliza watampata vipi.

Kwa taarifa yako hata Malaya hufikia wakati anataka apate mume atulie maishani.

Ujeuri weka pembeni!
ndivyo wanavyofanya waliodumu kwenye ndoa zao.

Usidanyike na fikra za wazungu eti usawa. Hakuna usawa Kati ya mume na mke Bali Kuna haki za mke na za mume. Tutakuwaje Sawa hali ya Kuwa maumbile yetu na uwezo wetu unatafautina hatuko Sawa.

Hao wazungu ndoa kwao si ajenda ya msingi maishani. Wamekuwa kama wanyama. Na hata waliomo katika ndoa maisha yao hayana tofauti na wasio kua na ndoa.

*Kuwa mnyenyekevu kwa mume sio kuwa mpumbavu. Bali ndio maumbile. Angalia hata kwa viumbe wengine. Panapotakiwa hekima na akili zitumie! Ndoa tamu kama hujui utamu muulize aliyekuwemo halafu akaiharibu kwa mikono yake. Akidhani Kuwa ataipata furaha nje ya ndoa. Halafu akaja kugundua Kuwa furaha aliicha kwa aliyekuwa mume wake. Halafu kurudi anataka lakini nafasi imechukuliwa na mwanamke mwingine.*

*Hebu fikiria.
 

Submission is the Ultimate Tool to Marital Happiness...
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23], pembe unawashikisha wote, mwenye nia atakuwa mvumilivu na mwisho wa siku atakamua maziwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…