Kwa sehemu kubwa ndege hiyo ya ATCL yenye injini mbili za jet, imeten-genezwa na Kampuni ya Boeing Commer-cial Airplanes ya nchini Marekani lakini injini zake zimetengenezwa na kampuni ya Rolls-Royce ya Uingereza.
Urefu wake ni mita 56.72, kimo kwenda juu ni mita 16.92 na upana wa mabawa yake ni mita 60.12, madirisha yake yana upana wa sentimita 27 kwa 47. Uwezo wa ndege hiyo mpya ni kubeba abiria 262 na mizigo yenye kilo za ujazo 136.7.
Kama kawaida ya ATCL, ndege zao hupambwa kwa rangi nyeupe na bluu huku picha ya mnyama twiga ikiwa kwa nyuma, maneno yanayosomeka ‘Air Tan-zania the wings of Kilimanjaro’ yamean-dikwa ubavuni mwa ndege zote za ATCL lakini imeongezewa lingine la ‘Hapa kazi tu