Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Hata hivyo, ligi hizi zilikuwa zimesimama kwa sababu ya kumalizika kwa msimu wa 2017-2018, hivyo watu wengi walizitumia Fainali za Kombe la Dunia 2018 kubeti na zenyewe zimeisha tangu mwezi wa saba.

Hivi sasa, mashabiki wa soka nchini na wale wanaoshiriki mchezo wa kubeti wameanza kufurahia tena kwani Ligi Kuu mbalimbali wanazozishabikia na zinazowapa fedha nyingi mojawapo ikiwa Ligi Kuu England zimeanza jana.
 
Hata hivyo, ligi hizi zilikuwa zimesimama kwa sababu ya kumalizika kwa msimu wa 2017-2018, hivyo watu wengi walizitumia Fainali za Kombe la Dunia 2018 kubeti na zenyewe zimeisha tangu mwezi wa saba.

Hivi sasa, mashabiki wa soka nchini na wale wanaoshiriki mchezo wa kubeti wameanza kufurahia tena kwani Ligi Kuu mbalimbali wanazozishabikia na zinazowapa fedha nyingi mojawapo ikiwa Ligi Kuu England zimeanza jana.
 
Ligi Kuu ya England (EPL) imeanza Agosti 10, 2018, Ligi Kuu ya Hispania (La Liga) inaanza Agosti 17, 2018, Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga) inaanza Agosti 24, 2018.

Pia kuna Ligi Kuu ya Italia (Serie A) inaanza Agosti 19, 2018 na Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1) ambayo imeanza jana Agosti 10, 2018. Zote watu wanasubiri kupiga pesa.
 
Kufanya mazoezi na kuushughulisha mwili mara kwa mara katika maisha yetu ya kila siku ni moja ya njia rahisi za kuufanya mwili kuwa imara kiafya.

Mazoezi yanatufanya kuwa na afya bora hivyo kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza ikiwamo magonjwa ya moyo, kisukari na unene uliokithiri.

Wengi wafanya mazoezi watu wazima huwa na nia ya kukabiliana na unene au uzito uliokithiri kwani husababisha matatizo ya kiafya.
 
Ni kawaida watu walio wengi hufanya mazoezi lakini hutajui tuna uzito kiasi gani au kutofahamu unene alio nao mtu upo katika kundi gani la uzito.

Ni muhimu sana kwa mtu yoyote yule hata asiye mfanyaji mazoezi kufuatilia kwa karibu mwenendo wa uzito wa mwili ili pale unapozidi kiwango cha kawaidi hatua za mapema zichukuliwe.

Kitaalam zipo njia kadhaa ambazo mara nyingi hutumika kubaini unene uliokithiri au kujua mtawanyiko wa mafuta yaliyorundikana mwilini.
 
Njia hizo na njia za kimahesabu kwa upimaji wa mzunguko wa kiriba tumbo na kugawa kwa urefu wa mwili hujulikana kama waist circumference ratio.

Njia ya pili ni waist-hip ratio yaani uwiano wa mzunguko wa kiriba tumbo na mzunguko wa paja na ya tatu ni Body Mass Index (BMI) ambayo ni ulinganishaji wa uzito na urefu wa mwili.

Njia ya BMI ndio inatumika zaidi kutathimini uzito wa mwili kwa watu wazima, siku ya leo nitaelenga zaidi njia hii kwani ndiyo inatupa taswira ya unene mwilini.
 
Kwa kawaida hutumia fomula ya kimehasibu kwa kugawa wa uzito katika kilogramu na urefu katika mita kipeuo cha pili. Mfano mtu mwenye Kilo 65 na urefu mita 1.5, BMI ni 70 gawa kwa 1.5 mara 1.5.

Kwa kutumia fomula vipimo vya uzito na urefu zao linalopatikana baada ya kukokotoa ndiyo hujulikana kama BMI, njia hii inatuwezesha kubaini kama ni unene uliokithiri au ni uzito mdogo sana.

Kwa mujibu wa shirika la Afya duniani-WHO BMI inatuwezesha kuanisha uzito wa mtu katika makundi matano. Jibu linalopatikana baada ya kukokotoa ndilo linatoa ainisho la uzito.
 
Kwa watu wazima BMI ya 18.5-24.9 kitabibu ni uzito salama kiafya, 25.0-29.9 hapa ni uzito mkubwa, 30.0-39.9 hapa huhesabika kama ni unene na 40.0 kuendelea ni unene uliokithiri.

Endapo BMI itakuwa chini ya 18.5 maana yake ni kuwa mtu huyo ana uzito mdogo sana.

Katika BMI hapa tunaweza kutofautisha uzito uliokithiri, unene na unene uliokithiri hivyo wataalam wa afya huitumia njia hii kutathimini hatari za kiafya wanazoweza kuzipata watu baada ya matokeo ya BMI.
 
Njia hiii ya BMI ni rahisi na haina gharama, ni njia ambayo inawezesha kubaini mrundikano wa mafuta mwilini na uzito uliokithiri kirahisi.

Makampuni ya simu za smart wana mfumo laini ndani ya simu wenye kikokotozi cha BMI unachokifanya ni kujaza tu uzito (Kg) wako na urefu wako kisha inakupa majibu (m). Ingawa BMI si moja kwa moja inapima mrundikano wa mafuta yote mwilini lakini ni kiashiria muhimu kuonyesha kuwa katika hatari ya kupatwa na magonjwa yasiyoambukiza.
 
Wakazi wa Dar es Salaam hivi sasa wanakumbana na uhaba wa kuku jambo ambalo linasababisha bei ya kitoweo hicho kupanda kwa asilimia zaidi ya 300.

Bei ya bidhaa hiyo katika masoko mbalimbali jijini hapa ikiwa ni pamoja na soko la Kisutu, Tegeta, Ilala na Shekilango, kwa wauzaji wa rejareja bei inaanzia Sh7,000 mpaka Sh8,000 kulingana na uzito tofauti na bei ya miezi mitatu iliyopita ambayo wastani ulikuwa Sh6,000.
 
Wauzaji wa jumla bei imeongezeka nakuwa Sh7,500 kwa wastani kutoka wastani wa Sh5,500 kwa miezi mitatu iliyopita.

Muuzaji wa jumla katika soko la Kisutu Abdulla Mohammed alisema kuongezeka kwa bei kunachangiwa na uhaba uliopo na gharama kubwa za bidhaa hizo kutoka kwa wafugaji.
 
Neema Justine ambaye ni mfugaji wa kuku alisema sababu kubwa ya kupanda kwa bei ya kuku ni kutokana na kuongezeka kwa gharama za uendeshaji kama kuongezeka kwa bei ya madawa na chakula.

“Bei ya chakula cha kuku kwa gunia la kilo 50 imeongezeka kutoka Sh60,000 hadi Sh65,000 lakini bei ya dawa za chanjo imeongezeka ndiyo maana hata bei ya mayai imepanda sasa hivi,” alisema Justine.
 
Hatimaye klabu ya Barcelona imesalimu amri kwa kuachana na mpango wa kutaka kumsajili kiungo mahiri wa Manchester United, Paul Pogba.

Mabingwa hao wa Ligi Kuu Hispania, wamesema walikuwa na nia ya kumsajili Pogba ili achukue nafasi ya Andres Iniesta aliyeihama timu hiyo baada ya kuitumikia kwa maisha yake yote ya soka.

Mkurugenzi wa michezo wa Barcelona, Ariedo Braida, alisema juzi kuwa wameachana rasmi na mpango wa kumsaili Pogba, lakini wanaendelea kusisitiza kuwa huyo ni mmoja wa wachache wachache walio bora zaidi duniani kwa sasa wa idara ya kiungo.
 
Barcelona imeachana na mpango wa kutaka kumsajili Pogba kwa sababu imekuwa vigumu kumpata, tumelazimika kukubaliana na hali halisi,” ilisema taarifa hiyo.

Imefichuka pia kuwa Barca ilimtengea kiungo huyo Pauni 180 za uhamisho, baada ya wakala wa mchezaji huyo Mino Raiola, kuketi nao na kuzungumzia uhamisho huo.

Klabu hiyo ilimshawishi Pogba na akakubali baada ya kuadiwa kiasi cha Pauni 10 milioni kwa mwaka nje ya mshahara wake wa kila wiki, wa Pauni 350,000 kwa wiki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…