Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

_*Happy Tuesday*_

[emoji208][emoji208][emoji208][emoji208]

*An elephant took a bath in a river and was walking on the road. When it neared a bridge, it saw a pig [emoji241][emoji241][emoji200][emoji200] fully soaked in mud coming from the opposite direction. The elephant quietly moved to one side, allowed the dirty pig to pass and then continued its onward journey.*

*The unclean pig later spoke to its friends in arrogance, “See how big I am; even the elephant was afraid of me and moved to one side to let me pass”.*

*On hearing this, some elephants questioned their friend, the reason for its action. Was it out of fear?*

*The elephant smiled and replied, “I could have easily crushed the pig under my leg, but I was clean and the pig was very dirty. By crushing it, my leg will become dirty and I wanted to avoid it. Hence, I moved aside.”*

*_This story reveals :_*
_*Realized souls will avoid contact with negativity not out of fear, but out of desire to keep away from impurity though they are strong enough to destroy the impurity._*

_*You need not react to every opinion, every comment, or every situation._*

_*Kick the drama and keep going ahead_*

*Choose your battles wisely... Not everything deserves Ur time and attention*

[emoji272][emoji272][emoji272][emoji272][emoji272]have a good day[emoji272][emoji272][emoji272][emoji272][emoji272][emoji272][emoji272][emoji272]
 
UNAJUA Ben Foster? Alishawahi kucheza Manchester United na sasa anaidakia Watford kwenye Ligi Kuu England.

Basi bana, Foster amewatazama makipa wote wa Ligi Kuu England na viwango vyao, kisa akasema kuna huyu David de Gea, yule ni Lionel Messi wa makipa.

De Gea, anatajwa kuwa kipa bora kabisa duniani, Jumamosi iliyopita kwenye mechi dhidi ya Watford, kipa huyo aliokoa hatari moja matata kweli kwenye dakika za majeruhi kusaidia timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 kwenye Ligi Kuu England.

“Yeye De Gea ni Messi wa makipa. Amekuwa kipa bora duniani kwa miaka mingi sana,” alisema.
 
HAYA ule utamu wa Ligi ya Mabingwa Ulaya umerudi tena. Safari hii mambo ni moto kwelikweli, maana ile hatua ya makundi tu inaanza, Liverpool inakipiga na Paris Saint-Germain.

Unaambiwa hivi, huo ni mtihani mzito kwa Kocha Jurgen Klopp, ambaye atapima kikosi chake kama kweli kipo vizuri kwa mapambano mazito baada ya kushinda mechi zake zote tano za kwanza kwenye Ligi Kuu England.

Mechi hiyo ngumu itapigwa leo Jumanne uwanjani Anfield, ambapo kutakuwa na shughuli nyingine pevu huko San Siro, wakati Inter Milan itakapoikaribisha Tottenham Hotspur.

Mechi nyingine kali itazishuhudia AS Monaco ikikipiga na Atletico Madrid, wakati Barcelona itakuwa na kibarua na PSV, huku Club Brugge ikiwa na kasheshe la kuikabili Borussia Dortmund na FK Crvena Zvezda itacheza na Napoli.

Kesho Jumatano kutakuwa na mechi nyingine kali kwelikweli, wakati Manchester City itakapocheza na Lyon, huku Real Madrid ikicheza na AS Roma. Man United nayo itaanzia ugenini kwa Young Boys, wakati Valencia itacheza na Juventus, huku Viktoria Plzen itacheza na CSKA Moscow na Shakhtar Donetsk itacheza na Hoffenheim. Kesho Jumatano pia kutakuwa na mechi kati ya Ajax itakayokuwa nyumbani kucheza na AEK Athens na Benfica itakipiga na Bayern Munich.
 
MAURIZIO Sarri ametamba ana uhakika supastaa wake, Eden Hazard atafunga mabao 40 na kubeba Kiatu cha Dhahabu kwenye Ligi Kuu England msimu huu.

Staa huyo wa Kibelgiji alifunga hat-trick wakati Chelsea ilipoibamiza Cardiff City mabao 4-1 Jumamosi iliyopita huko Stamford Bridge.

Kwa mabao hayo, Hazard amesaidia Chelsea kushika usukani wa Ligi Kuu England kutokana na kukusanya pointi 15 katika mechi tano ilizocheza na kushinda zote, huku staa huyo akiwa kinara pia kutokana na kuwa na mabao matano.

Msimu uliopita, Hazard alikomea kufunga mabao 12 tu kwenye mechi 34 alizocheza kwenye ligi, lakini Kocha Sarri anamini msimu huu atakuwa mfungaji bora.

“Nafikiria hivyo. Tumezungumza na nimemwambia anaweza kufunga mabao 40,” alisema Sarri wakati akijibu swali aliloulizwa kama anadhani Hazard atashinda Kiatu cha Dhahabu.
 
Anapaswa kujirekebisha baadhi ya vitu, lakini naamini anaweza kulifanya hilo.”

Lakini baada ya mechi, Kocha wa Cardiff City, Neil Warnock alisema Chelsea itapata shida sana itakapocheza na timu kubwa kutokana na beki yake ilivyo na jinsi inavyokabiliana na mashambulizi na Sarri amekubaliana na hilo, kuwa wana shida kwenye safu ya mabeki.

Msimu uliopita, staa wa Liverpool, Mohamed Salah ndiye aliyeshinda Kiatu cha Dhahabu na mabao yake 32.
 
LISEMWALO lipo wanasema, kama halipo basi laja. Akili ya Zinedine Zidane kwa sasa ipo kwenye kuinoa Manchester United tu, akionekana kukitamani kibarua hicho ambacho kwa sasa kipo chini ya Mreno, Jose Mourinho.

Zidane amekuwa akielezwa kuwa na mipango ya kukisuka upya kikosi hicho cha wababe wa Old Trafford, akiweka hadharani majina ya wachezaji anaowataka kuwasajili pindi atakapokamatia kibarua hicho.

Unaambiwa hivi, Zidane ameongeza mchezaji watano kwenye ile orodha ya wakali wake ambao anataka akitua tu Man United, basi nao wanaswe fasta ili kuifanya timu hiyo kuwa tishio na kuchuana na wababe wengine hasa mahasimu wao Manchester City katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England.
 
Lakini Zidane anataka kutengeneza timu itakayokuwa matata kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na kubeba mata makubwa.

Ripoti zinafichua Zidane anaitaka Man United imsajili staa wa Atletico Madrid na Ufaransa, Antoine Griezmann wakati atakapotua Man United na kuwaambia staa huyo ataigharimu United Pauni 178 milioni tu kupata huduma yake kama kipengele kinavyoelekeza kwenye mkataba wake huko Wanda Metropolitano.

Zidane hataki kutua Man United na kukuta kikosi cha kuungaunga na ndio maana amewataja mastaa wa maana ambao wote ni wachapakazi kama atawapata huko Old Trafford.

Wachezaji wengine wanne ambao Zidane atahitaji Man United ni Toni Kroos, James Rodriguez, Thiago Alcantara na Edinson Cavani.

Kama wachezaji hao wote wakitua Old Trafford, basi kuna wasiwasi mastaa kadhaa wa Man United kwa sasa itabidi wapigwe bei wakiwapo Paul Pogba, Nemanja Matic, Romelu Lukaku na hata Alexis Sanchez.
 
TUNAMWACHIA mwamuzi. Ndicho kitu ambacho Liverpool wamesema kuhusu tabia za Neymar za kujirusharusha ovyo uwanjani. Leo Jumanne wanamkaribisha katika dimba la Anfield katika pambano la Ligi ya Mabingwa wa Ulaya kundi C na huo ndio mkwara wao kwake.

Neymar alijipatia umaarufu zaidi wa tabia mbovu wakati wa fainali za Kombe la Dunia kule Russia kutokana na kujirusha mara kwa mara kiasi alidhihakiwa na mashabiki na wachezaji wenzake mitandaoni mara kwa mara. Staa huyo wa kimataifa wa Brazil alipumzishwa na kocha wake, Thomas Tuchel katika pambano dhidi ya Saint-Etienne wikiendi iliyopita lakini kabla ya hapo alipewa kadi ya njano kwa kujirusha katika pambano dhidi ya Nimes waliloshinda 4-2. Na sasa beki wa kushoto wa Liverpool, Andy Robertson ambaye pia anatazamiwa kukumbana na makali ya staa huyo wa zamani wa Barcelona amedai jukumu la kumshughulikia Neymar kwa kujirusha mara kwa mara wamemwachia mwamuzi wa pambano hilo, Cunety Cakir kutoka Uturuki.
 
Ubora wake unaongea mwenyewe. Ndiyo watu wanasema anaanguka chini kirahisi lakini hilo sio juu yetu. Ni juu ya mwamuzi kuamua. Tutakaa mbali na suala hilo. Sisi inabidi tuwe makini na ubora wake tu,” alisema Robertson.

“Kwa bahati mbaya katika suala la ubora ana ubora mwingi sana. Ndiye mchezaji ambaye inabidi atupe wasiwasi. Kitu kingine kibaya ni wana wachezaji wengi sana wenye ubora katika kikosi chao. Kitu kizuri kwetu ni kwamba tuna wachezaji wengi ambao wanaweza kuwaletea madhara,” aliongeza beki huyo ambaye kwa sasa amekuwa wa kudumu katika nafasi hiyo akimweka benchi Mhispaniola, Alberto Moreno.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…