Krimu ya Hydrocortisone ni dawa ya steroidi. Na hizi hupunguza kuvimba mwili, ugonjwa wa ngozi, kung’atwa na wadudu na eczema. Usipake dawa hii kwenye uso isipokuwa kwa maelekezo ya daktari.
Hii hutumika kwa ajili ya vidonda vidogo, michubuko na kuumwa na wadudu. Husaidia kuua bacteria na hivyo kidonda kupona mapema zaidi. m.f. hydrogen peroxide, spirit, iodine, polyhexanide, n.k.
Kuharisha huisha kwenyewe mara nyingi lakini inapozidi waweza kutumia dawa zifuatazo Loperamide(Imodium), Pepto-Bismol, Kaopectate, n.k.
Dawa hizi ni zaidi kwa ajili kutuliza maumivu na kutuliza dalili za ugonjwa. Muone daktari kwa ajili ya kupata tiba kamili hasa ukijikuta unahitaji kutumia dawa hizi mara kwa mara. Dalili huweza kuwa ishara ya ugonjwa mkubwa zaidi unaendelea kushamiri mwilini mwako.
Watu wenye magonjwa sugu kama asthma, kisukari, shinikizo la damu na mengineyo wahakikishe wanakuwa na dawa za ziada mara zote, usisubiri ziishe kabisa ndipo uende hospitali.