MFAHAMU DUMA !
Duma ni mnyama jamii ya paka, hutumia nyama kama chakula chake kikuu, usipokuwa makini unapomuona unaweza fikiri kwamba umekutana na chui, yote hiyo ni kwakuwa wana ufanano sana wanyama wa aina hii ya paka, hususani chui, simba malala (Tiger), chui mweusi (black pather) pia Jaguar na mondo.
Jike hubeba mimba kwa miezi mitatu, watoto hufungua macho baada ya siku 1 mpaka 3, na ifikapo mwaka mmoja na miezi sita, watoto hao huanza kujitegemea katika maisha yao, ingawaje bado huwa na ujilani na mama yao, Duma ni wanyama wasio na ushirikiano kabisa kutokana kutokuwa na utamaduni wa kuishi kifamilia kama ilivyo kwa simba.
Dume la duma kwa muonekano huwa na umbo kubwa kuliko jike, katika kundi la wanyama jamii ya paka hasa wale wakubwa, Duma ndio mnyama mnyonge wa mwisho, wembamba wake na uzito mdogo vinamfanya akose jeuri ya kupambana na wanyama wenzie wa aina moja kama chui, lakini si kwa wanyama wenzie tuu, bali hata ikitokea binadamu jasiri ukipewa kiboko kizuri cha kueleweka kama utamchalaza kimoja cha mgongo ni atakubali kushindwa tuu.
Chakula kikuu cha duma ni pamoja na nyani, mbuni, sungura, paa, ngiri,nyumbu, kudu, swala nk, tofauti na chui duma si kipenzi wa kula chakula juu ya mti, hivyo hukumbana sana na changamoto ya ugomvi wa fisi kung'anang'ana na chakula walichotafuta, na kwa timbwili la fisi hujikuta wao wakikubali kuwa wanyonge.