Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Meneja Manchester United Jose Mourinho anataka kumleta mlinzi wa Fiorentina Nikola Milenkovic. Mchezaji huyo wa kimataifa raia wa Serbia anawekewa thamani ya dola milioni 40 na klabu ya Italia kwa kuwa wanajua anawindwa na United, Tottenham, Chelsea, Arsenal na Juventus. (Star)
 
Meneja Mauricio Pochettino anasema Tottenham inataka kuwasaini wachezaji Januari, baada ya kutomsaini mchezaji yeyote wakati wa msimu wa joto. (Enfield Independent)
 
Mlinzi wa Real Madrid Marcelo, 30, anasema wachezaji wako chini ya shinikizo kutoka kwa meneja Julen Lopetegui baada ya kupata pigo lingine siku ya Jumamosi (Marca)
 
Nahodha wa klabu ya Juventus Giorgio Chiellini, 34, amemwambia kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba, 25, kwamba anakaribishwa tena katika klabu hiyo ya Itali.. (Mirror)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…