Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola amesema kuwa mchezaji wa Borussia Dortmund na Uingereza kinda Jadon Sancho huenda asirejee katika klabu hiyo katika kipindi chake cha ukufunzi. (Manchester Evening News)
 
Manchester City imeanza mazungumzo na winga Leroy Sane, 22, kuhusu kumuongezea kandarasi yake , licha ya kwamba raia huyo wa Ujerumani ana takriban miaka miwili na nusu iliosalia katika kandarasi (Telegraph)
 
Mwanamfalme wa Saudi Arabia Prince Mohammed bin Salman anatarajiwa kukutana na wamiliki wa Manchester United familia ya Glazer wiki chache zinazokuja, kuwasilisha ofa ya dola bilioni 4 kuinunua klabu hiyo. (Mirror)
 
Manchester City wanatathmini ofa ya pauni milioni 40 kwa mchezaji wa Bournemouth Nathan Ake mwezi Januari. Mchezaji huyo mwenye miaka 23 wa Uholanzi pia amehusishwa na Manchester United na Tottenham. (Sun)
 
Meneja Manchester United Jose Mourinho anataka kumleta mlinzi wa Fiorentina Nikola Milenkovic. Mchezaji huyo wa kimataifa raia wa Serbia anawekewa thamani ya dola milioni 40 na klabu ya Italia kwa kuwa wanajua anawindwa na United, Tottenham, Chelsea, Arsenal na Juventus. (Star)
 
Meneja wa Arsenal Unai Emery amekiri kuwa alikuwa anataka kumsaini mshambuliaji wa sasa wa Arsenal na Ufaransa Alexandre Lacazette mwanzo wa msimu wa mwaka 2016 - 2017 wakati akiwa meneja wa Paris St-Germain. (Mirror)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…