Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kilomoni awasapraizi wanachama
Katika hali ya kushangaza, mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini la Simba, Mzee Hamis Kilomoni jana alitinga kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere ambako kulifanyika Mkutano huo Mkuu wa Simba, na kushangiliwa na umati wa wanachama.
Mzee Kilomoni alikuwa ni miongoni mwa wanachama wa klabu hiyo ambao walikuwa wakipinga mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wake na ilifikia hatua hadi ya kufungua kesi mahakamani.
 
Umati wafurika mkutanoni
Tofauti na akidi iliyotangazwa awali kuwa mkutano huo utahudhuriwa na wanachama takribani 1,500, jumla ya wanachama 1728 walijitokeza kushiriki mkutano huo hali iliyopelekea kukosekana kwa viti vya kukalia na kusababisha wakae chini kufuatilia mkutano huo.
Pamoja na mshehereshaji (MC) kuwataka wanachama hao kutoziba njia zab ukumbi kwa kukaa chini, wanachama walipaza sauti wakimlalamikia MC kuwa hawana mahali pa kukaa hivyo waachwe wasibughudhiwe.
 
Ratiba yawachefua wanachama
Kuchelewa kuanza kwa mkutano mkuu wa Simba kuliwakera wanachama wa klabu hiyo ambao walidai ingewabana.
Ratiba ya kufungua mkutano mkuu ilionyesha kuanza saa 3:25 kwa Mwenyekiti kufungua mkutano mkuu ambayo ingefanyika hadi saa 6:30 mchana.
Hadi saa 4:15 asubuhi, mkutano haukuwa umeanza huku baadhi ya wanachama ambao waliomba hifadhi ya majina yao wakilalamika kuwa kuchelewa kuanza kwa mkutano huo kama ratiba ilivyopangwa kutasababisha waburuzwe Katiba baadhi ya ajenda hususani ya mapato na matumizi.
 
Tuna mkutano miwili, hadi sasa hakuna kinachofanyika, hii si dalili nzuri katika ajenda za mkutano mkuu kwani tuko nyuma ya muda na inaonyesha kuna baadhi ya ajenda hususani ya mapato na matumizi tutaburuzwa," alisema mmoja wa wajumbe ambaye aliungwa mkono na wenzake ndani ya ukumbini wa JNICC.
 
Vigogo kibao wahudhuria
Mbali na umati mkubwa ya wanachama waliohudhuria, viongozi na wadau wengi maarufu wa klabu hiyo walijitokeza kushiriki kwenye mkutano huo wakiongozwa na Kaimu Rais wa Simba, Salim Abdallah 'tRY Again', Zacharia Hanspoppe, Juma Kapuya, Hassan Dalali, Mulamu Nghambi, Hassan Hassanoo na wengineo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…