Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Marafiki wawili*(Elias na Ben)* walikuwa wanatembea mtaani akatokea mwanamke akarusha busu kwa mmojawapo kupitia dirishani katika jengo la ghorofa tatu. Wakaanza kujadiliana kama ifuatavyo: *Ben:* Muone yule mrembo amenirushia busu *Elias:* tafadhali achana na huyo mwanamke, usimjali.. _(baadae yule mwanamke akamuashiria aende)_ *Ben:* yule mwanamke ameniita! *Elias:* Rafiki yangu, usiende. Nakutafadhalisha. *Ben:* Kwa nini unaniambia nisiende Wakati mrembo kama yule ananiita? Huo ni wivu *Elias:* Ben, Ninakutafadhalisha tena, usiende, tafadhali usiende kule _(akihisi kutotiliwa maanani)_ _(Rafiki yake alimpuuza na alienda kwa yule mwanamke, mwanamke alishuka kukutana naye na wakapanda juu. Ghafla wakiwa wanataka kuanza taratibu za kula uroda, wakasikia mlio WA gari getini)_ .. πŸ”ŠπŸ”Š *Lady:* _(akiangalia kupitia dirishani)_ Oooh! Yule ni mume wangu!! *Ben:* Mama yangu ! Nipo matatani, kweli ? ..!! *Lady:* Usiwe na khofu, jifanye kuwa Dobi na anza kupiga pasi hizo nguo (akimuonyesha lundo la nguo) _(Ben alitumia masaa matano kukamilisha kunyoosha zile nguo kwa sababu yule mume hakutoka tena siku ile)_ _(Siku iliyofuatia Ben alikwenda kwa Rafiki yake)_ *Ben:* Kaka, unaweza kuamini Jana nimepiga pasi nguo kwa masaa matano??? *Elias:* Lakini nilikwambia usiende. Nguo zote hizo ulizonyoosha, *Nilizifua Mimi Juzi!!* πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ *When an experienced person speaks ... πŸ‘‚you must listen..!*
 
Wadada wa siku hizi wanaona bora kumuachia House girl mtoto mdogo anayenyonya,ye akaenda kazini na moyo ukawa na amani kabisa. Kuliko kumuacha House girl huyo huyo na Mume,hata akisafiri kwa siku Mbili. πŸ˜‚πŸ˜‚iπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ™ŒπŸ»πŸ™ŒπŸ»πŸ™ŒπŸ»
 
Mtumishi wa MUNGU mmoja akiwa kwenye gari alisimamishwa na Trafic Police,police akiwa anahitaji rushwa alianza kuuliza maswali mengi, mara mbona gari lako linatoa moshi mwingi? mbona gari lako matairi yameisha, hatimaye polisi akamuamuru padre waende nae kituoni. Njiani polisi alimuuliza , umesema wewe ni Mtumishi wa MUNGU, je unabiblia ndani ya gari, akajibu ndio ninayo, polisi akamuambia , pack ...gari pembeni na unipe biblia. Mtumishi akapaki gari na kumpa biblia yule polisi,Polisi akasita kupokea, akamwambia Mtumishi 'fungua na usome Mathayo 5:25-26 "Mtu wa Mungu akasoma ": "Patana na Mshtaki wako upesi,wakati uwapo pamoja naye njiani: yule mshtaki asijekukupeleka kwa kadhi na kadhi akakupeleka kwa askari,ukatupwa gerezani. " Amin nakuambia,Hutoki humo kamwe hata uishe kulipa senti ya mwisho" Mtu wa Mungu akampa yaliyo yake kaizari. Polisi akatabasamu na kusema 'msifanye migumu mioyo yenu".. Enenda kwa amani
 
Bibi alienda kupiga Xray, Doctor akamwambia moyo umetoboka katikati na pembeni umevimba pande mbili. Bibi akasema we mtoto wewe nadhani umechanganya negative ya picha ya mtu alipiga matako yake? Nenda kalete ya kwangu
 
Mzee mmoja aliwakataza vijana kuvuta bangi karibu na nyumba yake,Wavuta bangi wakaamua kumwamisha huyo mzee nanyumba yake,kwanza wakavuta bangi ya kutosha wakavua mashati wakaanza kusukuma ile nyumba, kibaka akapitia yale mashati, mmoja wao alivyogeuka nyuma hakuyaona akajua wameshafika mbali akawaambia wenzie tukazane tumefika mbali hata nguo zetu hazionekani wakaendelea mpaka bange zilivyoyeyuka kchwani wakaona wako palepale.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…