Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Endapo itathibitika pasipo shaka kwamba Mwalimu Michael Ikila ameishi tena kinyumba na mwanafunzi yuleyule aliyewahi kuelezwa kukutwa akiishi naye, basi usemi wa “Sikio la kufa halisikii dawa” utasadifu kwake.
 
Mwalimu huyo wa Shule ya Sekondari Nyakasungwa, Buchosa wilayani Sengerema alikamatwa Septemba 21 akituhumiwa kuendelea kuishi kinyumba na mwanafunzi wake akiwa bado yuko chini ya uchunguzi kwa kosa hilo. Mwanafunzi huyo alihitimu kidato cha nne mwaka 2016 na kuchaguliwa kujiunga na kidato cha tano katika Shule ya Sekondari Mkinga, Tanga mwaka 2017 lakini hakuripoti baada ya kuanza kuishi kinyumba na mwalimu hiyo. Baada ya kukamatwa kwa kosa hilo, Mwalimu Ikila alitakiwa kuripoti polisi kwa uchunguzi zaidi.
 
Wakati uchunguzi dhidi yake ukiendelea na kutakiwa kuripoti polisi, ilielezwa kuwa Mwalimu Ikila na mwanafunzi huyo waliamua kuondoka Sengerema na kuhamishia makazi yao Mtaa wa Nyamazobe, Mwanza na kukamatwa juzi.
 
Akizungumza na Mwananchi kuhusu suala hilo, Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Emmanuel Kipole alisema taratibu za kumfikisha mahakamani mwalimu huyo zinaendelea.

“Lazima aadhibiwe kwa mujibu wa sheria kwa sababu kitendo chake sio tu kinakiuka maadili na miiko ya ualimu, bali pia ni uvunjifu wa sheria,” alisema Kipole.
 
Ofisa Elimu wa Halmashauri ya Buchosa ya Wilaya, John Busiga alisema pamoja na mtuhumiwa kufikishwa mahakamani, mwanafunzi huyo atarejeshwa shuleni na atalazimika kukariri kidato cha tano.

Ofisa Elimu Mkoa wa Mwanza, Michael Ligola aliyefanikisha mtuhumiwa kutiwa mbaroni alisema tayari ofisi yake kwa kushirikiana na vyombo vingine imeanzisha uchunguzi wa kina kuhusu tuhuma za baadhi ya walimu wilayani Sengerema kudaiwa kujihusisha kingono na wanafunzi wao.
 
Mama mzazi wa mwanafunzi huyo, Maria Kimbambeze aliyezungumza kwa simu juzi, alisema mtoto wake alianza kuishi kinyumba na mwalimu huyo baada ya kutoroshwa mara tu alipomaliza mitihani ya kidato cha nne mwaka 2016.

“Baada ya kumaliza mitihani na matokeo kutoka kuwa anatakiwa kuendelea na kidato cha sita, familia ilishindwa kumudu kumlipia gharama; kitendo hicho kilimfanya mtoto kubaki nyumbani kabla ya kutoshwa na mwalimu wake kwenda kuishi naye kama mume na mke,” alisema.
 
Ni wazi kuwa kanuni mpya za Sheria ya Hifadhi ya Mifuko ya Jamii ya mwaka 2018 zimeibua maswali mengi kwa wananchi.

Mathalani, wapo wanaohoji juu ya sababu za kupunguzwa kwa ulipwaji wa mafao kutoka asilimia 50 mpaka 25 kwa mkupuo.

Pia, wapo wanaohoji kiasi cha fedha kurejea serikalini baada ya mstaafu kufariki dunia, ikiwa ni baada ya wategemezi wake kulipwa mafao yake ya miaka mitatu.
 
Wengine wanahoji kuhusu kujitoa licha ya ukweli kuwa hakuna aina hiyo ya mafao. Baadhi wanajiuliza kwa kanuni hizo, nani atapata na nani atakosa kati ya watumishi wa sekta binafsi na serikalini. Pia, kuna wanaohoji baada ya kuunganishwa kwa mifuko ya hifadhi ya jamii watapataje mafao yao ikiwa walichangia katika mifuko miwili tofauti.

Wanaodai mafao yao wamebaki na sintofahamu juu ya malipo yao kama yatafanyika kwa kutumia kanuni na sheria ya zamani au mpya.
 
Sababu kupunguzwa

mafao ya mkupuo

Akijibu maswali hayo juzi, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Irene Isaka alisema ukokotoaji huo si mpya kwani ulianza tangu mwaka 2014 kwa mifuko yote isipokuwa kwa wanachama wa PSPF, GEPF na LAPF wa kabla ya Julai Mosi 2014. Lakini sasa lengo ni kuweka usawa kikokotoo miongoni mwa wanachama ili wawe wanachangia kwa kiwango kipya.
 
Licha ya kuwa wanachama wote wa mifuko wanachangia asilimia 20 ya mshahara, lakini mafao ya mkupuo yalikuwa yanatofautiana kulingana na mfuko anaotumia. Baada ya tathmini tulikuja na kikokotoo ambacho kinaweza kuboresha mafao ya wanachama na kuimarisha sekta ya mifuko ya hifadhi ya jamii,” alisema Isaka.

Kwa mabadiliko ya sasa, wanachama wa mifuko yote ya hifadhi ya jamii watakuwa wakipewa mafao mkupuo kwa asilimia 25 tofauti na awali ambako wale wa mifuko ya watumishi wa umma walikuwa wakipewa mafao ya mkupuo ya asilimia 50.
 
Miaka mitatu mstaafu

akifariki

Isaka alisema mifuko ya hifadhi ya jamii utaratibu wake ni kama wa bima kwamba watu wanakusanya pamoja lakini fedha anapewa mwenye uhitaji kwa wakati huo ndiyo maana kuna wanaopata pensheni kwa miaka 28 na wengine mwaka mmoja tu.

“Baada kupata mafao ya mkupuo ambayo ni asilimia 25, mstaafu ataendelea kulipwa asilimia 75 ya pensheni ambayo itagawanywa kwa kila mwezi kwa kipindi chote cha maisha yake na atakapofariki familia yake itapata pensheni ya miezi 36 (miaka mitatu),” alisema Isaka akitoa mfano wa mtumishi ambaye mshahara wake wa mwezi ni Sh442,000 kwamba endapo atachangia kwa miaka 32, jumla ya michango yake itakuwa Sh8.64 milioni, lakini mafao yake ya mkupuo yatakuwa Sh10.81 milioni na kila mwezi atakuwa akilipwa Sh216, 293 maisha yake yote, na akifa familia yake itapata Sh7.78 milioni (pensheni ya miezi 36) hata kama atakuwa amelipwa pensheni kwa miaka 20 au zaidi.
 
Nani anapata/anapoteza

Kulingana na maelezo ya SSRA, hakuna mtu anayepoteza, lakini wanachama wa LAPF, GEPF na PSPF ambao awali walikuwa wanapata mafao ya mkupuo ya asilimia 50, sasa mkupuo wao utapungua kwa asilimia 25 (nusu) lakini pensheni yao ya kila mwezi itaongezeka.

“Kiwango kilichopunguzwa hapo ni mkupuo tu. Fedha zake zimeongezwa kwenye pensheni ya kila mwezi. Bado tunawalinda watu wenye kikokotoo kikubwa, kwa wanachama wa PSSSF bado kikokotoo chao ni 1/540 na wanauza wastani wa kuishi 15.5,” alisema.

Alisema malalamiko yaliyopo yanatokana na watu wachache waliokuwa na mikopo ya nyumba kwa kuwa wakati PSPF ikitoa mkupuo wa asilimia 50 mwanachama alikuwa anaruhusiwa kukopa nyumba hadi asilimia 25 ya mkupuo wake. Alishauri wanachama hao washauriane na mifuko yao, lakini si kubadilisha sheria wala kanuni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…