Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

.WASIWASI umetanda katika viunga vya Old Trafford kwamba huenda Manchester United isimalize nafasi nne za juu mwishoni mwa msimu huu baada ya mwendo wa kusuasua wa timu yao katika Ligi Kuu ya England mpaka sasa.
 
United Jumamosi ilitoka suluhu ya bila kufungana na Crystal Palace katika dimba la Old Trafford na sasa imeachwa nyuma kwa pointi saba na Chelsea ambayo inashikilia nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 28 huku wapinzani wengine wa Top Four Arsenal wakiwa na pointi 27.
 
Suala la ubingwa linaanza kuonekana kuwa ndoto kwa United ambayo kwa sasa imeachwa pointi 14 na viongozi wa Ligi hiyo, watani wao wa jiji la Manchester, Manchester City ambao wanaonekana kupambana zaidi na Liverpool katika msimamo wa Ligi.
 
Desemba hali ya United inaweza kuwa mbaya kwa sababu wana mechi mbili ngumu dhidi ya Arsenal Desemba 5 na pia wanalazimika kucheza na Liverpool Desemba 16. Mpaka sasa United imeambulia pointi moja tu kutoka kwa wakubwa watatu ambao wamecheza nao Tottenham, Chelsea na Manchester City.
 
Ingawa katika karatasi mechi nyingine ni dhidi ya Southampton, Fulham, Cardiff, Huddeslfied na Bournemouth zinaweza kuonekana kuwa rahisi lakini suluhu dhidi ya Palace imethibitisha kwamba United bado haipo sawa.
 
Katika pambano dhidi ya Palace, United walionekana kuvurugukiwa uwanjani na staa wa zamani wa United, Paul Ince alimshukia vikali kocha wa United, Jose Mourinho huku akidai kwamba mpaka sasa hakijui kikosi chake cha kwanza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…