Wakati United inaposhindwa kufunga, unamuingiza Fellaini, unacheza mipira mirefu, Palace wanajiandaa kwa hilo. United wanategemea bahati.” Alisema Ince.
Kumlipa Sanchez nusu ya pauni milioni moja kwa wiki kwa ajili ya kucheza eneo la nyuma na kupiga mipira mirefu? Hatumtaki awe hivyo. Tunamtaka awe katika eneo la 18. Mashabiki wamekuwa na uvumilivu lakini muungano wa kitimu au namna ambayo tunataka kucheza.” Aliongeza Ince.
Mourinho hana uhakika na kikosi chake cha kwanza, kila wakati kinabadilika mara kwa mara kama Fulham. Baada ya kuwepo hapa kwa miaka mitatu huku akitumia mamilioni ya pauni bado haijui timu yake.
Ukiwa kama kocha hili upate muunganiko wa kitimu na mwendelezo wa ubora unahitaji kuwa na kikosi cha kwanza unachokiamini. Wachezeshe mechi tano na wataweza kucheza vizuri zaidi.” Alisema staa huyo wa zamani.
Kesho United wanarudi kibaruani katika michuano ya Ligi ya Mabingwa kukipiga na Young Boys katika uwanja wao wa Old Trafford na Jumamosi ijayo watasafiri ugenini kukipiga na Southampton katika pambano la Ligi Kuu.
Jumatano ijayo wanatazamiwa kuwa na kibarua katika uwanja wao wa nyumbani kucheza na Arsenal ambayo imebadilika zaidi msimu huu tangu kuingia kwa kocha mpya, Unai Emery aliyechukua mikoba ya Arsene Wenger.