Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ninaamini Jumapili ijayo ‘leo’ mtaiona timu tofauti na muonekano wa siku za hivi karibuni, tutawapa Arsenal wakati mgumu uwanjani, naamini baada ya wiki mbili hatutapoteza tena mchezo na watu watatushangaa,” aliahidi wiki iliyopita.
 
Walioilaza Arsenal na majozi leo ni Danny Ings dakika ya 20 na 44, kabla ya Charlie Austin kuihakikishia ushindi katika dakika ya 85, wakati mabao yote ya Arsenal yalifungwa na Henrikh Mkhitaryan dakika za 28 na 53.
 
Kwa ushindi huo bila shaka mashabiki wa Southampton wataupongeza uongozi wa klabu yao kwa kumpa jukumu hilo kocha Ralph Hasenhuttl raia wa Austria kwani amethibitisha atakuwa mkombozi wa timu hiyo.
 
Kwa upande wake kocha wa Arsenal, Unai Emery, alisema mchdezo umekuwa mgumu kuliko walivyotarajia na akawapongeza vijana wake kwa kupambana wakitoka nyuma mara mbili kabla ya kufungwa bao la tatu dakika ya 85.
 
Ushindi huo umeiwezesha Chelsea kuendelea kung’ang’ania nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi Kuu England, ikifikiza pointi 35 mbili nyuma ya Tottenham iliyo nafasi ya tatu na saba nyuma ya vinara Manchester City.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…