Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Hatimaye Mourinho ametimuliwa baada ya kuwa na msimu mbaya katika klabu hiyo na muda wowote atatangazwa kocha wa muda atakayekuwa na timu hadi mwisho wa msimu. Michael Carrick anapewa nafasi kubwa ya kupewa jukumu hilo kwa sasa.
 
Man United inategemea kumtangaza kocha wa muda ndani ya saa 48 zijazo.

Kocha mpya atakayekuja atakuwa na jukumu la kuhakikisha Man United inatwaa ubingwa iliyosubiri kwa muda tangu walipofanya hivyo msimu wa mwaka 2013.
 
MAKOCHA WANAOTAJWA KUTUA MANCHESTER UNITED

10/11 - Zinedine Zidane

4/1 - Antonio Conte

5/1 - Mauricio Pochettino

5/1 - Laurent Blanc

14/1 - Arsene Wenger

22/1 - Leonardo Jardim

25/1 - Mikel Arteta

33/1 - Massimiliano Allegri

33/1 - Eddie Howe

33/1 - Ryan Giggs

33/1 - Brendan Rodgers

33/1 - Diego Simeone

33/1 - Roberto Martinez

33/1 - Luis Enrique

33/1 - Didier Deschamps

40/1 - Carlo Ancelotti

50/1 - Thomas Tuchel

50/1 - Michael Carrick

50/1 - Rafa Benitez

66/1 - Marco Silva

66/1 - Gareth Southgate

75/1 - Sean Dyche

75/1 - Eric Cantona

Odds according to Betfair
 
Kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Liverpool Jumapili iliyopita kimehitimisha kibarua cha kocha Jose Mourinho katika klabu ya Manchester United.

Katika mchezo ambao Liverpool walikuwa nyumbani kwenye Uwanja wa Anfield, Mwenyekiti na mtendaji Mkuu wa Klabu hiyo, Ed Woodward, alikuwa uwanjani pembeni mwa gwiji la soka la klabu huyo Sir Bobby Charlton.
 
Ed Woodward alikuwa akitingisha kichwa kuashiria kutoridhishwa na kilichokuwa kikiendelea uwanjani wakati wote wa mchezo huo, hasa ikizingatiwa kuwa alimuacha nje kiungo Paul Pogba aliyenunuliwa kwa ada iliyovunja rekodi ya Paundi 89 milioni kutoka Juventus mwaka 2016
 
Hii ni mara ya pili kwa Mourinho kutimuwa ndani ya mwezi huu, tena baada ya kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Liverpool ikumbukwe alitimuliwa Desemba 17 mwaka 2015 na Chelsea wakati akiinoa kwa mara ya pili, sababu ikiwa ni kipigo na matokeo mabaya kwa ujumla.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…