Ray Parlour na Karen (1998-2001
Parlour alimuoa mke wake, Karen mwaka 1998. Waliachana mwaka 21 wakiwa na watoto watatu. Julai 2004 walikubaliana kumaliza mzozo wa masuala ya pesa ambapo ilikubalika Karen apewe nyumba mbili na kiasi cha Pauni 250,000 lakini hawakukubaliana katika suala la pesa ya malezi. Parlour aliahidi kutoa kiasi cha Pauni 120,000 kwa mwaka kwa madai ingetosha kwa mahitaji ya watoto na mwanamke lakini hata hivyo Karen alitaka zaidi. Mahakama ilitaka Parlour atoe kiasi cha Pauni 212,000 kwa mwaka lakini pande zote hazikukubali. Karen aliona ndogo wakati Parlour aliona kubwa.