Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Klabu ya Chelsea imemsaini mshambuliaji wa Borussia Dortmund Christian Pulisic kwa dau la Yuro 64m lakini itamtoa kwa mkopo kwa klabu hiyo ya Ujerumani hadi mwisho wa msimu,
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 raia wa Marekani , ambaye alikuwa amehusishwa na vilabu vya Liverpool na Arsenal , alijiunga na Dortumund akiwa mchezaji mchanga 2015.
Pulisic amefunga magoli tisa katika mechi 23 akiichezea Marekani.
''Ilikuwa ndoto ya Christian kujunga na ligi ya Uingereza'' , alisema mkurugenzi wa klabu ya Dortmund Michaek Zorc.
 
DIRISHA la usajili wa majira ya baridi huko Ulaya limeshafunguliwa mwezi huu w Januari na tayari timu zimeanza kufanya kweli kunasa mastaa wapya ikiwamo West Ham United waliombeba staa wa zamani wa Arsenal na Manchester City, Samir Nasri.
 
Usajili ni jambo moja na kuja kutamba kwenye kikosi ni jambo jingine. Kwenye Ligi Kuu England hawa hapa ndio mastaa walionaswa kwenye usajili uliopita, ambao huduma zake zimekuwa tamu kinoma. Kwa kifupi tu, huu ndio usajili bomba wa dirisha lililopita huko kwenye Ligi Kuu England.
 
Jorginho - Chelsea
Staa muhimu kabisa kwenye kikosi cha Maurizio Sarri huko Chelsea. Kiungo, Jorginho amekuwa na umuhimu wake kwenye msimu wake wa kwanza kwenye kikosi hicho cha Stamford Bridge. Mtaliano huyo bado hajafika kwenye kiwango cha ubora wake unaofahamika, lakini kwa kuanza amekuwa na mwanzo mzuri na hakika ni moja ya mastaa wapya waliofanya kweli kwenye chama la Chelsea.
 
6.James Maddison - Leicester City
Kiungo huyo mpya wa Leicester City, James Maddison ameikamatia si mchezo Ligi Kuu England na hilo linaonekana kwa kiwango chake cha ndani ya uwanja. Mwanzoni wakati ananaswa na wakali hao wa King Power, Maddison alionekana kuwa ni mchezaji wa kawaida tu kabla ya sasa kufanya mambo makubwa na kutambulika kwamba ni mmoja wa usajili bora akifunga mabao matano na asisti tatu.
 
5.Kepa Arrizabalaga - Chelsea
Uhamisho wa Thibaut Courtois kwenda Real Madrid uliwaacha Chelsea kwenye mashaka makubwa sana kabla ya kupata mtu sahihi wa kuja kuziba pengo la kipa huyo wa Kibelgiji. Chelsea ilitoa Pauni 71.6 milioni kumsajili kipa Kepa Arrizabalaga kutoka Athletic Bilbao. Tangu alipotua kwenye Ligi Kuu, Kepa amefanya mambo matamu, akiwa na rekodi ya kucheza mechi nane bila ya kufungwa.
 
4.Xherdan Shaqiri - Liverpool
Kiufundi, Liverpool haikuwa ikihitaji huduma ya mchezaji kama Xherdan Shaqiri kwenye kikosi chao, lakini kocha Jurgen Klopp anahitaji kuwa na kikosi kipana. Aliona washambuliaji wake Mohamed Salah na Sadio Mane wanahitaji mtu wa kuja kuwasaidia na ndio maana akafanya usajili huo. Shaqiri ameonyesha kuwa muhimu, akifunga mabao sita na kuasisti mara mbili kwenye Ligi Kuu England.
 
3.Felipe Anderson - West Ham
Wakati West Ham United walipovunja rekodi yao ya usajili walipolipa pesa kibao kumnasa Mbrazili, Felipe Anderson, wachambuzi wa soka walihoji sana hilo. Anderson alinaswa kama mrithi wa Dimitri Payet na hakika baada ya kutua tu kwenye Ligi Kuu England amefanya mambo makubwa kweli. Tayari staa huyo amefunga mabao manane na kuasisti mawili kwenye Ligi Kuu England.
 
2. Lucas Torreira - Arsenal
Kwa mechi zilizochezwa kwenye Ligi Kuu England hadi sasa, kiungo Lucas Torreira ameonyesha kwanini mashabiki wa Arsenal walifurahi sana wakati aliposajiliwa. Torreira ametua Arsenal kwa ada ya Pauni 26 milioni akitokea Sampdoria na tangu wakati huo shughuli yake imekuwa pevu ndani ya uwanjani. Anakaba na anafunga mabao, akifunga mara mbili na asisti mbili kwenye ligi.
 
1.Alisson - Liverpool
Huduma yake iliwagharimu Liverpool, Euro 62.5 milioni walipomnasa kutoka AS Roma. Na hakika, kipa Alisson ameonyesha uhalali wa kusajiliwa kwa pesa nyingi hivyo kutokana na huduma yake anayofanya kwenye goli la Liverpool. Kwenye mechi alizocheza kwenye Ligi Kuu England, kipa huyo amekuwa golini kwenye mechi 12 bila ya kuruhusu bao katika Ligi Kuu England.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…