Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Umenikumbusha kisa hiki kilichosisimua sana wakati ule.
Namkumbuka bi Simbaulanga, maana aliolewa na mwanafamilia furani jirani yetu.
Pia huyu Toroha Mohamed Toroha alikua na ofisi binafsi ya ujanjaujanja mtaa wa Aggrey/Jamuhuri Kitumbini Dsm, kwenye hotel ya Sleep Inn. Mzaramo huyu Bagamoyo wa Bagamoyo alikua mtoto wa mjini kwelikweli. Kisa hiki na kile cha Kapteni Azizi Abdallah vilishangaza sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Moto wa Gesi Waua Mama na Watoto wake Wawili Mwanamke mmoja aliyetambuliwa jina la Pendo Adolph Manyama (29) na watoto wake wawili, wakazi wa Kola katika Manispaa ya Morogoro, wamefariki dunia baada ya nyumba yao kuungua na moto uliyosababishwa na kulipuka kwa jiko la gesi. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Wilbrod Mutafungwa, alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea Desemba 26, mwaka jana, saa 10:30 jioni , maeneo ya Kola, Manispaa ya Morogoro. Mutafungwa alisema siku hiyo mtoto wa mama huyo aliyejulikana kwa jina la Angela Baltazar (4) alifungua mtungi wa gesi na kusababisha gesi kujaa ndani ya nyumba hiyo. “Wakati mtoto akifungua mtungu huo, mama yake ambaye alikuwa Mwalimu wa shule ya Msingi Forest, bila kujua aliingia ndani na jiko la mkaa na kusababisha moto kulipuka na kumuunguza yeye na watoto wake wawili, jambo lilosababisha vifo vyao,” alisema. Aidha, Kamanda Mutafungwa aliwataka wananchi kuwa waangalifu wakati wote wanapokuwa wanatumia vyombo hivyo vya majumbani, ili kuepusha ajali mbalimbali za moto kutokea. Mmoja wa jamaa wa karibu na familia hiyo, alielezea tukio hilo lilitokea Jumatano iliyopita wakati mume wa mama huyo, Baltazar Kineneko (37) akiwa mkoani Arusha kikazi. “Ilikuwa majira ya usiku mama akiwa anapika kibarazani kwenye jiko la mkaa mtoto wa miaka minne aliingia ndani na kuchezea jiko la gesi, gesi ikawa inavuja. "Mtoto alipofungua mlango kutoka nje mvutano wa gesi na mkaa ulisababisha mtungi wa gesi kulipuka hadi juu na kutoboa gypsum. “Mama aliingia ndani kumuokoa mtoto, lakini alitoka akiwa anaungua mwili mzima. Mtoto wake mwingine wa miaka sita aliyekuwa nje anacheza alipoona mamaye anatoka ndani na mdogo wake huku wakiwa wanaungua moto alikimbia kumkumbatia mama yake naye akaanza kuungua,” alieleza jamaa huyo. Ndugu huyo alisema mama na mtoto mdogo walikufa papo hapo, mtoto mkubwa alisafirishwa kwa ndege kwenda Nairobi nchini Kenya kwa matibabu baada ya hali yake kuonekana mbaya. Hata hivyo, jamaa huyo alisema baba wa mwanamke aliposikia kuwa mwanaye na mjukuu wamekufa alipata mshtuko naye akafa hapo hapo,R.I.P
 
Tukio la kusikitisha sana aisee!!
Rest In Peace.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wamepita njia ya maumivu makali. Kibinadamu huwa tunakufuru kwa kumuuliza Mungu "ulikuwa wapi wakati yanatendeka haya?"
Mimi ni nani hata nikamkosoa Mungu.
Hakika maandiko yametimia,kila nafsi itaonja mauti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…