Kumbuka kuwa yaliyopita yamepita, yawezekana umewahi kufanya jambo fulani ukashindwa hapo awali, fumba macho usitazame matokeo ya nyuma, anza upya na utafanikiwa. Mara nyingi watu hutumia matokeo ya nyuma kufanya maamuzi ya sasa na ya baadae na wengine utasikia wanasema, mbona fulani alifanya na akashindwa, na wewe pasipokufikiri kwa umakini kuwa ni yeye lakini wewe utaweza kufanikiwa.