Barcelona imesema iko tayari kupokea ofa ya kumnunua kiungo wao wa kati Philippe Coutinho, 26.
Manchester United imeonesha nia ya kumsaini mchezaji huyo wa zamani wa Liverpool wakati wa msimu wa joto. (Calciomercato, via Star)
Barcelona pia wameweka dau la pili la kumnunua winga wa Chelsea na Brazil, Willian, baada ya ofa yao ya kwanza ya kumnunua kiungo huyo wa miaka 30 kugonga mwamba siku ya Alhamisi. (Standard)
Chelsea imekubali kuwanunua kwa masharti viungo wa kati Nicolo Barella, kutoka klabu ya Cagliari na Leandro Paredes, 24, wa klabu ya Zenit St Petersburg. (Telegraph)
Meneja wa AC Milan Gennaro Gattuso amesema kuwa klabu hiyo inaendelea kuzungumza na wawakilishi wa mshambuliaji Gonzalo Higuain licha ya tetesi kuwa mshambuliaji huyo huenda akahamia Chelsea. (Express)