Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kocha wa Monaco, Thierry Henry amesema hatakuwa adui kwa muda na bosi wa Nice, Patrick Vieira wakati nyota hao wa zamani wa Arsenal na Ufaransa watakapokutana kwa mara ya kwanza wakiwa makocha.
 
Vieira alikuwa kocha wa Nice mwezi Juni, kabla ya Monaco kumpa jukumu Henry mwezi Oktoba.

Wawili hao watakutana leo usiku katika mchezo wa Ligue 1, baada ya mechi hiyo awali kuhairishwa kutokana na sababu za maandanamo ya watu wanaopiga serikali ya Ufaransa.
 
Vieira ni rafiki yangu ni mtu ninayemkubali sana," alisema Henry.

"Siyo tu kwa uchezaji wake, lakini hata katika maisha yake, na mchezo huu hautabadilisha chochote.

"Lakini leo ni mechi kati ya Monaco dhidi ya Nice ni mchezo muhimu, kwa sababu hiyo hatutoweza kupenda."
 
Kiungo Paul Pogba na mchumba wake Maria Salaues walionekana wakitoka kupata chakula cha jioni katika mgahawa wa The Ivy jana usiku baada ya wawili hao kupata mtoto kwa mara ya kwanza.
 
Gwiji wa Old Trafford, Bryan Robson aliimbia Sportsmail wiki hii kuwa: 'Wakati alipomuona Paul wiki iliyopita Dubai na kikosi cha Man United, nilimpa hongera kwa kufanikiwa kupata mtoto.
 
Alioneka akiwa ametulia kama hakuna kilichotokea.'

Wapenzi hao walionekana wakitembea pamoja kutoka katika mgahawa huo wa jijini Manchester huku wakisindikizwa na rafiki yao.
 
Salaues alionekana akiwa na tumbo kubwa mwishoni mwa mwaka huu alipojitokeza uwanjani kumtazama Pogba akichezea Manchester United kwenye Uwanja wat Old Trafford kabla ya mwaka mpya.
 
Mchumba wake Salaues alionekana akiwa mwembamba huku amevalia gauni lake zuri, wakati Pogba alikuwa amevaa tracksuit nyeupe juu na suruhali ya jeans nyeupe.
 
Kwa mara ya kwanza wawili hao walijulikana kuwa wanamahusiano wakati mrembo huyo alipoituma picha ya kumpongeza Pogba baada ya kuisaidia Ufaransa kutwaa ubingwa wa Kombe la Dunia Russia mwaka jana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…