Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ligi ina ushindani mkubwa, hii ni klabu ya kihistoria, na Rafa Benitez mwenyewe ndio sababu niko hapa leo.
"Nadhani ni jukumu kubwa, jambo linalopendeza, na nitajaribu kufanya kila niwezalo kulipa imani ambayo klabu inayo kwangu."
 
Miguel Almiron ni nani?
Almiron amechangia ushindi mara 13 kwa Paraguay na amefunga magoli 13 msimu uliopita wakati Atlanta iliposhinda taji la MLS kwa mara ya kwanza.
Mshambuliaji huyo amefunga magoli 21 katika mechi 62 za ligi alizocheza, akiwa amewahi kuichezea Cerro Porteno nyumbani na timu ya Argentina Lanus.
Aliwahi pia kuwa bingwa wa ligi ya Argentina mnamo 2016 baada ya kuicheza Lanus mechi 12 katika divisheni ya Primera.
 
Uhamisho wa Miguel Almiron kuingia Newcastle unamfanya kuwa mchezaji ghali zaidi kuuzwa kutoka ligi kuu ya soka Marekani.
"Tulikuwa tunamfukuzia Miguel Almiron kwa muda," amesema meneja wa Newcastle Rafael Benitez. " Tuliona mchezaji aliye na kasi katika ushambuliaji, anayeweza kucheza nyuma ya mshambuliaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…