Katika mchezo huo Paris St-Germain ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia Angel Di Maria, ambaye shuti lake lilimpita Anthony Lopes na kujaa wavuni dakika saba.
Mshambuliaji chipukizi Vinicius Junior alifunga bao na kuonyesha soka ya kiwango cha juu wakati Real Madrid ikijiandaa na mchezo wa katikati ya wiki wa El Clasico dhidi Barcelona baada ya kuichapa Alaves mabao 3-0.
Pia imepunguza tofauti ya pointi na mahasimu wao Barcelona kubaki nane. Miamba hiyo ya Hispania itakutana kwa mara ya kwanza mwaka huu katika nusu fainali ya Kombe la Mfalme Jumatano hii.
ROMAN Abramovich huwa hataki masikhara na pesa zake. Muda wowote anaamua anachoamua bila ya kusita. Na sasa inadaiwa kwamba kimya kimya ameelekeza nguvu zake katika kumchukua kocha wa Tottenham, Mauricio Pochettino msimu ujao.
Tayari kocha wa Chelsea, Maurizio Sarri ameanza kukalia kuti kavu baada ya Chelsea kuondoka katika mbio za ubingwa huku akiwa katika hatihati ya kuendelea kubaki Top Four licha ya ushindi wa mabao 5-0 wa Chelsea dhidi ya Huddersfield juzi.
Inasemekana kwamba Sarri amelazimika kumtumia meseji tajiri huyo wa Kirusi kufafanua jinsi fomu ya timu hiyo ilivyopotea baada ya kuchapwa mechi mbili za ugenini mfululizo dhidi ya Arsenal na Bournemouth Jumatano iliyopita.