Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Sharti la kwanza la Zidane ni kuhakikishiwa staa wa Chelsea, Eden Hazard atabakishwa klabuni hapo wakati huu ambao inasemekana amekata shauri kuondoka Stamford Bridge baada ya kuchoshwa na maisha ya klabu hiyo.
 
Hazard ni mmoja kati ya mastaa wanaowindwa na klabu ya zamani ya Zidane, Real Madrid na inadaiwa klabu hiyo imeandaa kitita cha Pauni 100 milioni kwa ajili ya kumtwaa staa huyo wa kimataifa wa Ubelgiji, ambaye anaonekana kama mmoja kati ya watu ambao watapunguza maumivu ya Madrid kuondokewa na Cristiano Ronaldo katika dirisha kubwa la mwaka jana.
 
Sharti la pili ambalo Zidane amewapa Chelsea ni kumuandalia dau la Pauni 200 milioni kwa ajili ya kukifumua tena kikosi hicho ambacho msimu huu kinaonekana kusuasua na Zidane hataki kufanya kazi na baadhi ya mastaa wa sasa wa Chelsea.
 
Kiasi hicho cha pesa pia kitatokana na mauzo ya baadhi ya mastaa wa sasa kama vile Willian ambaye amekuwa mguu ndani mguu nje na msimu uliopita alitakiwa na Barcelona kwa dau la Pauni 65 milioni lakini bado Chelsea iligoma kumuuza.
 
Zidane pia ametoa sharti la tatu ambalo ni kuachiwa maamuzi ya manunuzi na mauzo ya wachezaji sambamba na Mkurugenzi wa ufundi wa sasa wa Chelsea, Marina Granovskaia ambaye kwa sasa ana kauli ya mwishoni klabuni hapo akiwa ameaminiwa na tajiri, Roman Abramovich.
 
Hata hivyo licha ya masharti hayo, Zidane anaamini Sarri bado anaweza kuendelea kuwa kocha wa Chelsea msimu ujao kama ataweza kurekebisha mambo ikiwemo kushinda pambano gumu la jana dhidi ya Manchester United michuano ya FA na pia kutwaa taji la Kombe la Ligi ambapo wanatazamiwa kucheza na City mwisho wa mwezi huu.
 
Zidane pia anaamini kibarua hicho kinaweza kuota mbawa kwake endapo tu Sarri atafanikiwa kuiingiza Chelsea katika Top Four licha ya upinzani mkubwa uliopo baina ya Chelsea, Manchester United na Arsenal katika mbio za kuisaka nafasi hiyo.
 
Mpaka sasa kwa mujibu wa Sarri, tajiri Abramovich hajawasiliana naye kufuatia kichapo cha aibu cha mabao 6-0 ambacho Chelsea walipokea wiki iliyopita kutoka kwa Manchester City ugenini lakini ni wazi kichapo hicho kimeanza kuashiria mwanzo wa mwisho wake Stamford Bridge.
 
Sarri ambaye alichukuliwa kutoka Napoli katika dirisha kubwa lililopita kuziba pengo la kocha aliyetimuliwa, Antonio Conte, amekuwa akilalamika wachezaji wake wamekosa hamasa ya kusaka ushindi tofauti na ilivyokuwa katika siku za mwanzo ambapo kikosi chake kilikuwa mwendo mdundo na ilionekana kama vile kingefanya makubwa msimu huu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…