Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

[emoji16][emoji16][emoji16]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MAURIZIO Sarri. Kitu ambacho anaweza kukifanya kwa sasa ni kukusanya tu mabegi yake kujiweka tayari kwa ajili ya kusubiri kufukuzwa tu. Kichapo kingine chochote kitakachofuatia, hasa kwenye ile mechi ya fainali ya Kombe la Ligi dhidi ya Manchester City, haiwezi kukiacha salama kibarua chake huko Stamford Bridge.
 
Bilionea Roman Abramovich hatazamwi kama ataendelea kuwa na uvumivu baada ya hapo. Kitu kingine ni kwamba hata gharama za Sarri kufukuzwa kazi ni ndogo kuliko za makocha wengine wote waliowahi kufanya kazi kwenye kikosi cha Chelsea na kufukuzwa. Kinachoelezwa ni kwamba Sarri akifukuzwa, fidia atakayolipwa ni Pauni 5 milioni tu.
 
Hiyo ni fidia ndogo zaidi kuwahi kulipwa kwa makocha wote waliowahi kufanya kazi kwenye kikosi cha Chelsea chini ya bilionea huyo wa Russia. Sarri atalipwa fidia ndogo kuliko hata aliyolipwa Avram Grant, wakati alipofukuzwa 2008, ambapo alilipwa Pauni 5.5 milioni.
 
Makocha wengine waliolipwa pesa zinazokaribia na hizo ni Claudio Ranieri, ambaye alilipwa Pauni 6 milioni mwaka 2004 sawa na ilivyokuwa kwa Carlo Ancelotti alipotimuliwa mwaka 2011, ambapo alipewa mkwanja wa Pauni 6 milioni.
 
Hizi hapa fidia kubwa zaidi Abramovich aliwalipa makocha waliokuja kuinoa Chelsea baada ya kuwafuta kazi. Kwa ujumla wake, Abramovich ametumia Pauni 89.3 milioni kulipa makocha aliowafukuza kazi.
 
Antonio Conte – (2018, Pauni 9 milioni)

Mtaliano, Antonio Conte ndiye wa mwisho kufutwa kazi huko Chelsea baada ya mambo kwenda kombo. Kocha huyo alifukuzwa Julai 2018 na nafasi yake kuja kuchukuliwa na Sarri. Wakati Conte anafungasha virago vyake na kuondoka Stamford Bridge alilipwa fidia ya Pauni 9 milioni.
 
Jose Mourinho – (2015,Pauni 9.5 milioni)

Mreno, Jose Mourinho kwa sasa anahusishwa tena na mpango wa kurudi Chelsea na hiyo itakuwa mara ya tatu. Mara mbili alizokuwa kwenye timu hiyo, zote alifukuzwa kazi. Awamu yake ya pili, alifukuzwa kazi Novemba 2015 baada ya timu kufanya hovyo. Hata hivyo, jambo hilo limemwingizia pesa Mourinho, kwani alilipwa Pauni 9.5 milioni fidia.
 
Roberto Di Matteo – (2012, Pauni 10.7 milioni)

Staa wa zamani wa Chelsea, Roberto Di Matteo alirudi kuinoa timu hiyo Machi 2012, lakini hadi kufika Novemba 2012 akafutwa kazi. Miezi yake minane aliyokuwa kwenye timu hiyo, Di Matteo aliisaidia timu kubeba taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya. Di Matteo alianza kama kocha wa muda, kabla ya kupewa mkataba wa kudumu na alipofukuzwa kazi, alilipwa fidia ya Pauni 10.7 milioni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…