Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Supastaa huyo wa Arsenal amekuwa na imani kwamba alitengwa na chama cha soka cha Ujerumani wakishindwa kumtetea kutokana na mashambulizi ya maneno yaliyokuwa yakielekezwa kwake kisa tu kupiga picha na Erdogan mwaka jana.
 
Ozil ana asili ya Uturuki na alishutumiwa kufanya kampeni za chinichini kumsaidia rais huyo kuchaguliwa tena, licha ya yeye mwenyewe kusisitiza kwamba mazungumzo yake aliyofanya na rais huyo yalikuwa yakuhusu mpira tu.
 
Baada ya picha yake aliyopiga na Erdogan kuibuka, kiungo huyo alikuwa akizomewa na mashabiki wa Ujerumani kwenye fainali za Kombe la Dunia 2018, ambapo timu hiyo iliyokuwa mabingwa watetezi walishindwa kutamba na kutupwa nje kwenye hatua ya makundi tu.
 
Grindel alitaka kiungo huyo funsi wa mpira aondoshwe kwenye kikosi cha Ujerumani kabla ya fainali za Kombe la Dunia 2018 hazijaanza kwa sababu tu ya picha yake aliyopiga na Rais wa Uturuki, picha ambayo pia iliwahusisha kiungo wa Manchester City, Ilkay Gundogan na staa wa Everton, Cenk Tosun.
 
Bosi huyo wa FA ya Ujerumani hadharani alimtuhumu Ozil kuwa ndio chanzo cha timu yao kuboronga kwenye fainali za Kombe la Dunia, jambo lililomfanya staa huyo wa Washika Bunduki kudaiwa Grindel alikuwa akimsakama tu kwa chuki.
 
Licha ya kulipa kodi Ujerumani, kuchangia vifaa mbalimbali vya shule, kushinda Kombe la Dunia 2014 nikiwa na Ujerumani, bado haitoshi kukubalika kwenye jamii na badala yake nachukuliwa tofauti.
 
Staa Ozil hivi karibuni alifanya kitendo ambacho kimefichua wazi uhusiano wake mbovu na wakali wawili Mats Hummels na Thomas Muller baada ya kuamua kumpongeza Jerome Boateng peke yake kwa kustaafu soka la kimataifa wakati wakali hao wote watatu walitangaza kustaafu kwa wakati mmoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…