Mungu Atuepushe na misukosuko katika siku ya leo [emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji42][emoji25][emoji42][emoji25][emoji42][emoji25][emoji2221][emoji2221][emoji2221]
Usingizi wenye afya ni moja ya kiungo muhimu sana kwa maendeleo ya afya nzuri kwa kila mtu, ukweli ni kwamba kama hupati usingizi wa kutosha na mazuri basi afya yako itadorora na utakuwa ni mtu wa kuumwa kila siku.
tutaangalia baadhi ya mambo yanayopelekea kukosa usingizi na ushauri sahhi na rahisi wa kufuata ili kurudisha usingizi wako mazuri na ukafurahisa Maisha.
Usingizi mzuri wenye afya ni upi?
Hili ni swali muhimu na la kwanza kujiuliza pale unapoanza safari yako ya kurudisha usingizi mwanana na kuepuka adha ya kukosa usingizi huku ukihesabu makenchi.
Dr Naiman ambaye ni mwanasaikologia kutoka Marekani anasema “usingizi siyo tu ni kitendo cha kutokuamka, hii ni tafsiri isiyo sahihi miongoni mwa watu kwenye dunia yetu kwa sasa. Tunatafsiri usingizi kinyume na mana halisi.
na hivyo tunaamini kufumba macho na kutoamka ni usingizi huku ikiwa siyo kweli, anaendelea kusema kuna baadhi ya vigezo ni lazima vizingatiwe tunapoongelea usingizi wenye afya.
Jinsi gani tatizo la kukosa usingizi huanza.
Kukosa usingizi ama kupata usingizi wa shida na kuchelewa kupata usingizi ni moja ya matatizo makubwa yanayosumbua watu kwa kipindi hiki, kila siku tunapokea wagonjwa wengi wanaotafuta ushauri jinsi gani warudishe usingizi ,mnono wa mwanzo ili waweze kufuahia Maisha.ili kufahamu kwanini hupati usingizi basi ni muhimu kujua uhusiano kati ya kiwango cha usingizi na usumbufu/kelele.
Kiwango cha usingizi: kikawaida uwezo wa kusinzia unatakiwa e kuwe unaongezeka kadiri siku inavoisha, yaani kadri jua linavochwea basi uwezo wa kusinzia huwa unaongezeka na kuwa mkubwa Zaidi wakati usiku unapoingia.
Usumbufu/kelele: usumbufu/kelele ni kitu chochote ambacho kinaharibu ama kuingiia usingizi. Kama kiwango cha usumbufu/kelele kikiwa kikubwa kuliko uwezo wa kusinzia basi ni wazi kwamba utapata shida kusinzia. Usumbufu/kelele zinaweza kuwa kwenye aina tatu, usumbufu/kelele za kimazingira, usumbufu/kelele za kimwili na usumbufu/kelele za `kiakili.
Mchana mwili unakuwa na nguvu na ukiwa na motisha kubwa ili kufanya shuguli zako za kimaendeleo, lakini hali hii inapojitokeza wakati wa usikku basi yatakiwa kutambua kuwa kuna tatizo na tutaita ni usumbufu/kelele.
Aina mojawapo ya usumbufu/kelele ambazo huingilia Zaidi usingizi kwa watu wengi ni mfululizo wa fikra mbalimbali ambazo zinakuwa zinazunguka kwenye akili wakati wa usiku na hivo kuingilia upatikanaji wa usingizi mtamu.
Mifano ya usumbufu/kelele za kimwili ni kama maumivu ya viungo, shida kwenye umen`genyaji wa chakula, madhara ya matumizi makubwa ya vidonge, na mabaki ya caffeine iliyotokana na unywaji wa kahawa nyakati za jioni
Kwanini ni muhimu kulala kwenye giza nene (complete darkness)
Uwepo wa mwanga kwenye chumba chako cha kulala kinaingilia uzalishaji wa kichocheo cha melatonini ambacho huusika katika kukufanya usinzie. Kupungua kwa uzalishaji wa homoni ya melatonin huweza kuleta athari kubwa kwa afya ya mtu ukiachilia mbali kuharibu usingizi
Mfano utafiti unasema kuna uhusiano mkubwa kati ya upungufu wa melatonin na kuongezeka kwa hatari ya kuugua saratani ya matiti. Miaka ya nyuma kabla teknologia haijakua mababu zetu walilala masaa 12 wakiwa gizazi kabisa, leo hiii kutokana na uvumbuzi wa umeme na taa, tumejikuta masaa 16 tukiyatumia kwenye mwanga na masaa 6 tu tukitumia kwenye giza na tena pakiwa mwanga hafifu kwa nje ukiendelea kuwaka.