Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Messi amezusha wasiwasi kutokana na maumivu yake ya nyonga. Staa huyo ameripotiwa kujitonesha maumivu hayo ya siku nyingi kwenye mechi ya kimataifa wakati alipoitumikia Argentina iliyochapwa 3-1 na Venezuela kwenye mechi ya kirafiki iliyofanyika juzi Ijumaa jijini Madrid. Kutokana na maumivu hayo, Messi amelazimika kurudi Barcelona kupatiwa matibabu.
 
Kutokana na hilo Messi hatakuwapo kwenye mechi nyingine ya kirafiki ambapo, Argentina itamenyana na Morocco kesho kutwa Jumanne. Barcelona wamelazimika kumwondoa haraka kwenye kikosi hicho cha timu ya taifa ili asiumie zaidi wakati mbele yao kuna mechi ngumu ya kuwakabili Man United kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.
 
Messi, 31, alicheza kwa dakika zote 90 katika mechi yake hiyo ya kwanza kurudi kuitumikia Argentina baada ya kuwa nje kwa siku 265 baada ya kichapo kile cha mabao 4-3 kutoka kwa Ufaransa kwenye fainali za Kombe la Dunia 2018. Lakini, Venezuela alitibua ujio wake mpya kwenye soka la kimataifa baada ya kuikandamiza Argentina 3-1 na sasa amewatia presha Barca juu ya ufiti wa afya yake.
 
Wakali hao wa Nou Camp pia wapo kwenye shaka kubwa juu ya mshambuliaji wao mwingine, Ousmane Dembele. Bila shaka, Man United watakuwa wanapiga sala kuhakikisha washambuliaji hao wote wanashindwa kurudi kwenye ubora wao wakati wanashuka uwanjani kukabiliana na vinara hao wa La Liga.
 
Barcelona ilitoa taarifa yake ya staa wao Messi kukatisha uwepo wake kwenye mechi za kimataifa kutokana na kupata majeruhi hayo na hivyo, hatakuwapo katika mechi dhidi ya Morocco akirudi klabuni kwa uangalizi zaidi.
 
Messi amekuwa kwenye kiwango bora kabisa kwa siku za karibuni, akiongoza Barca vyema kushinda 5-1 katika mechi ya pili ya hatua ya 16 bora kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Lyon, ambapo staa huyo alifunga mara mbili na kuasisti mara mbili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…