Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Katika kesi ya awali mwaka jana, bwana Short alidai kuwa hakumbuki kujamba akiwa karibu na Hingst lakini "yawezekana ilitokea mara moja ama mbili hivi, yawezekana."
Hata hivyo, alikanusha kuwa alifanya vitendo hivyo "kwa madhumuni ya kumkera na kumbughudhi" Hingst.
 
Hingst alikuwa akimuita Short "Bwana Mnukaji" na alikuwa akipuliza uturi kila aliposogea karibu yake, korti iliambiwa.
Kwa mujibu wa mitandao ya Australia, Hingst amedai kuwa, tabia ya Short ilikuwa ni sehemu ya mpango wa kumng'oa kazini na muda aliofanya kazi na Construction Engineering kulimsababishia majeraha ya kiakili. Pia amedai kuwa Short alikuwa akimkejeli kutokana na ufanisi wake na kumpachika jina la "bwege".
 
😀😀😀😀
 
Mshambuliaji wa Brazil Neymar yumo katika mazungumzo ya kuongeza mkataba na klabu yake ya Paris St-Germain, kwa mujibu wa baba wa mchezaji huyo. Mshambuliaji huyo mwenye miaka 27 amekuwa akihusishwa na mipango ya kuhamia Real Madrid. (ESPN)
 
Benfica wanataka kuongeza kipengele kigumu kwenye mkataba wa mshambuliaji Mreno Joao Felix ili kuzipunguza makali klabu ambazo zinzmnyemelea mshambuliaji kinda huyo. Manchester United na Juventus zimekuwa zikihusishwa na kumtaka Felix, 19. (Tuttosport - in Italian)
 
Kiungo wa Manchester United raia wa Uhispania Ander Hererra, 29, amesema ni jambo la kawaida kuhusishwa na kutaka kuhamia klabu ya Paris St-Germain kutokana na kusalia miezi mitatu tu mpaka mkataba wake na Old Trafford kufikia tamati. (El Periodico - in Spanish)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…