Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

IJUE MIFUMO YA SOKA NA ILIPOTOKEA.
Mifumo ya soka inayotumika sasa imepitia historia ndefu sana ikibadilika mara kwa mara kutokana na maendeleo makubwa katika " mbinu" na " ufundi " wa mchezo huu pendwa zaidi duniani.
 
Mfumo mama ambao umezaa mifumo yote inayotumika katika soka na iliyowahi kutumika na kuachwa ni 1-2-7 ambao ulitumika sana katikati ya 1800s lakini mwishoni mwa karne hiyo ( 19th ) ulifanyiwa marekebisho na kuzaliwa 2- 3 - 5.
 
Lakini baada ya ufahamu kuongezeka katika elimu ya soka hususani katika tacticts and techniques ( mbinu na ufundi) baadhi ya majina kama " half back " pale kati yaliondoka na kuanza kutumia majina kama midfield ( destroyer or defensive midfield) .
 
Hii iliyokea sana miaka ya 1970s. Miaka ambayo mapinduzi makubwa katika mbinu , mifumo na aina ya uchezaji vilifanyika katika soka. Hiki ndicho kipindi dunia ilishuhudia wadachi wakiingia katika soka na patterns mpya za " total football". Uligeuka mfumo mama ulaya mashariki.
 
Total football ilikuja kukinzana na samba la kibrazil lililohasisiwa vyema na uboreshaji wa mfumo wa 4-2-4 na kuibuka kwa 4-3-3 lakini wazo likianzia kwa kwa waalimu wa Uruguayi ambao waliujaribu mfumo huo mwaka 1950 . Brazil waliingia na 4-3-3 kwa mara ya kwanza katika kombe la dunia mwaka 1962 na kuonekana moto wa kuotea mbali
 
Mfumo unaoruhusu umilikaji mzuri wa mpira, kasi , kutawala eneo la kiungo, kushambulia pande zote na kuwalazimisha wapinzani muda wote kujilinda na kukosa muda wa kuwashambulia kutokana na pressing yenu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…