BEKI Gerard Pique amemwokoa Diego Costa asikumbane na adhabu kubwa zaidi baada ya straika huyo wa Atletico Madrid kutolewa kwa kadi nyekundu katika mchezo wa kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Barcelona.
Costa alionyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja katika dakika ya 27 baada ya kumtolea lugha chafu Mwamuzi, Jesus Gil Manzano. Kadi hiyo nyekundu ilimkasirisha Costa na kuonekana kutaka kugomea kutoka uwanjani, lakini ghafla Pique akawahi na kumziba mdomo kumzuia staa huyo mwenzake wa kimataifa wa Hispania asizungumze maneno zaidi ambayo yatamtia kwenye matatizo makubwa.
Jambo hilo halina maana kwamba litamfanya Costa asikabiliane na adhabu ndefu zaidi huku kukiwa na madai anaweza kukosa hadi mechi nane msimu huu. Wachezaji wenzake bila ya shaka watakuwa na hasira naye kutokana na kuwafanya wacheze pungufu kijinga na kupoteza mchezo huo.
KOCHA wa Real Madrid, Zinedine Zidane ameshindwa kukanusha uwezekano wa Gareth Bale kuondoka kwenye timu hiyo mwishoni mwa msimu huu baada ya mashabiki wa Los Blancos kuzidi kumzomea staa huyo.
Winga huyo wa zamani wa Tottenham alizomewa sana na mashabiki wa Madrid kwenye mechi dhidi ya Eibar, ambapo Los Blancos ilitoka nyuma na kushinda 2-1 uwanjani Bernabeu. Straika, Karim Benzema alifunga mara mbili kwenye kipindi cha pili, lakini Madrid itaendelea kubaki kwenye nafasi ya tatu katika msimamo wa La Liga.
Bale, 29, alikuwa adui mkubwa uwanjani hapo, ambapo pasi zake zote, alipogusa mpira au kupiga shuti jambo hilo lilipokewa kwa kelele za kuzomewa kutoka kwa mashabiki wa Madrid. Akizungumzia hatima ya Bale, Zidane alisema: “Tutaona.
“Sitasema nini kitatokea. Yupo hapa Madrid na ana mkataba wa miaka miwili au mitatu imebaki. Huu sio muda wa kulizungumzia hilo. Hatufurahishwi na kelele za kuzomea, lakini mashabiki wanataka timu yao ifanye vizuri.”
Bale amehusishwa na kuihama timu hiyo kwenye dirisha lijalo la usajili, lakini shida ni hakuna timu yoyote kwenye Ligi Kuu England iliyo tayari kumudu mshahara wake wa Pauni 650,000 kwa wiki. Ripoti kutoka huko Hispania zinadai Zidane yupo tayari kumtema staa huyo wa zamani wa Tottenham