Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Lakini, kama unavyofahamu wachezaji ni kama bidhaa sokoni, inapokuwa nzuri hata thamani yake inakuwa kubwa, lakini inapokuwa na kasoro kidogo tu thamani zao sokoni zinashuka.
 
Rodrigo – Valencia,

Euro 20 milioni

Straika wa Valencia, Rodrigo amekuwa akitamba kwenye La Liga kwa miaka michache ya karibuni. Staa huyo Mhispaniola kuna kitu kwenye soka lake, lakini kwa siku za karibuni ubora wake wa uwanjani umekuwa duni. Akiwa na umri wa miaka 28 baada ya kuwa kwenye kiwango bora, Rodrigo amekuwa tofauti na jambo hilo limeporomosha thamani yake sokoni kwa kiasi kikubwa sana.
 
Diego Costa – Atletico,

Euro 20 milioni

Kwenye siku zake, Diego Costa anakuwa mshambuliaji hatari sana, hashikiki uwanjani. Lakini, kwa siku za karibuni, yale makali ya Costa yamekuwa hayapo tena. Amekuwa akiandamwa na majeruhi pia jambo lililomfanya apungue ule moto wake wa kupasia mipira nyavuni. Katika msimu huu huko kwenye La Liga, straika huyo mwenye umri wa miaka 30 amefunga mara mbili tu kuonyesha kwamba ameshuka ubora na hivyo hata thamani yake sokoni kushuka pia.
 
Thamani yake ya sasa:

Euro 40 milioni

Thamani yake Desemba 21,

2018: Euro 60milioni

Kiwango alichoshuka:

Euro 20 milioni
 
Lionel Messi –

Barcelona,

Euro 20milioni

Huyu ni staa ambaye hajaathirika kutokana na ubora wake wa uwanjani. Lionel Messi shida pekee iliyoshusha thamani yake sokoni ni umri wake kuwa mkubwa, miaka 31 na hivyo inapunguza ile kasi yake ya asili ndani ya uwanja. Lakini, staa huyo bado ameendelea kuonyesha ubora wake ndani ya uwanja akifunga mabao 44 kwenye michuano tofauti aliyocheza msimu huu huku akihusishwa kwenda kubeba Ballon d’Or kwa mara ya sita.
 
Marcelo –

Real Madrid, Euro 35milioni

Umekuwa msimu usiokuwa na mvuto huko Real Madrid, ambapo beki wao wa kushoto maarufu kabisa, Marcelo kucheza chini ya kiwango. Marcelo amekuwa akicheza chini ya kiwango tangu mwanzoni mwa msimu na matokeo yake amejikuta akiishia kukaa kwenye benchi tu. Hata hivyo, bado ni mchezaji muhimu licha ya kwamba na kuwa na umri mkubwa, lakini kiwango chake duni kimeshusha thamani yake sokoni.
 
Philippe Coutinho –

Barcelona, Euro 40milioni

Mambo hayaendi vizuri kwa Philippe Coutinho tangu alipotoka Liverpool kwenda kujiunga na Barcelona, Januari 2018. Kocha wa Barcelona, Ernesto Valverde, amempatia Coutinho muda wa kutosha tu kuonyesha ubora wake
 
lakini Mbrazili huyo ameshindwa kufanya kile kilichokuwa kikitarajiwa na wengi wakati aliponaswa kwa pesa ndefu. Mechi 29 alizocheza kwa La Liga, amefunga mara tano tu na kuasisti mara mbili jambo lililomfanya thamani yake sokoni kushuka kwa kiasi kikubwa sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…