Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Na tujue kwamba kwenye ubinafsi na choyo hatuwezi kujenga vyote hivi. Kama tunataka kuendelea kama taifa ni lazima tubadilike kutoka ndani yetu kwenda nje.
Kama hatupendi vita ni lazima tuangalie haya mambo kwa umakini. Ni lazima tujenge mahusiano yetu na kutumikiana.
 
Vitu kama ufisadi na mambo mengine ni matokeo ya watu kuacha maisha ya kijamii na kujiangalia wao tu na kujilimbikizia mali, hasa kwa viongozi na watu wengine kwa njia ambazo si halali na kuacha kujali jamii ambazo wanatoka, na ambazo zinawategemea wao kuleta mabadiliko chanya. Huu ni uasi. Uasi dhidi ya jamii. Na uasi huu ukitendwa na viongozi jamii yote hukengeuka na kuwa ya kibinafsi. Hatuwezi kujenga nchi katika ubinafsi na nchi ikawa imara.
 
Kubomoka kwa maisha ya kijamii ni madhara makubwa yatokanayo na ubinafsi na choyo. Hatujali tena shule za serikali za pamoja ambazo ni muhimu, zinazopaswa kutoa elimu bora kwa wote. Kwakuwa uhai wa taifa lolote unakuwepo pale tu watu wake wote, wanapopata elimu bora ambayo haina matabaka na jamii inapoangaliwa kwa ukaribu katika ukuaji wake kiroho na kiakili, kwasababu binadamu si mali peke yake; lazima aangaliwe ukuaji wake wa kiroho na kiakili ambao humfanya kuwa na afya bora ya mwili.
 
Ama sivyo tutajenga watu ambao wanafikiria tu kupata elimu na kuitumia elimu hiyo kwa maslahi binafsi pekee. Na hili sio lengo la taifa kusomesha watu wake. Malengo ya taifa kusomesha watu wake ni maendeleo ya pamoja kama nchi na kutatua changamoto zinazokabili maisha ya binadamu hasa maisha ya raia wa taifa hili. Ni kufanya watu au wasomi kitumia akili zao sio kutengeneza matatizo bali kutatua changamoto zinazotukabili. Sio kufanya ujanja ujanja na ulaghai.
 
Hii roho ya kujitolea tunawajibika kuijenga kwa watu wetu. Watu lazima wasome, na lengo lao liwe ni kuendeleza taifa lao, na sio kufikiria zaidi maslahi binafsi kuliko yale ya kitaifa. Ni jukumu letu kujenga taifa la watu wanaowajibika kwa nchi yao.
 
Tunaona tatizo hili pia kwenye siasa zetu, watu kujifikiria wenyewe kuliko maslahi mapana ya taifa. Na niaminini; tutaendelea zaidi kama tutaachana na ubinafsi, tukasikilizana kwa lengo la kuendeleza taifa letu. Sisi ni watu wamoja na tuna lengo moja maendeleo ya nchi yetu. Lakini ubinafsi ndio uliotugawa na kuturudisha nyuma kwenye maendeleo y
 
Tumegawanyika kimawazo sio kwasababu ya kutofautiana kifikra kuhusu njia bora za kuendeleza taifa hili, bali kwasababu za ubinafsi wa uchu wa mali na madaraka. Tunatakiwa tubadilishe mtizamo wetu na kulipa taifa hili kipaumbele kuliko matamanio yetu binafsi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…