Miongoni mwa njia ambazo zinakua kwa kasi sana kwa hivi sasa katika suala la kutangaza biashara ni pamoja na kutumia mitandao ya kijamii ( social networks).
Pamoja na kuwapo kwa mitandao hii ya kijamii wengi wao wemekuwa wanatangaza pasipo kujua namna ya kutangaza na kitendo hiki kinawafanya watu hao wakose wateja huku wakizidi kutangaza biashara zao katika mitandao.
Binafsi nimekuwa nikiona watu wakitangaza bishara zao huku wakisema nauza kitu fulani kwa maelezo zaidi naomba unifuate inbox au tuwasiliane kwa namba hizi.
Unachotakiwa kufanya;
Ili uweze kuwapata wateja wengi kwa kupitia mitandao ya kijamii unatakiwa kueleza faida za bidhaa atakazozipata mteja pindi atakaponunua bidhaa husika.
Naomba nirudie tena kwa kusema "ili Ili uweze kuwapata wateja wengi kwa kupitia mitandao ya kijamii unatakiwa kueleza faida atakazozipata mteja pindi atakaponunua bidhaa husika.
simu hii ina uwezo mkubwa wa kukaa na chaji kwa muda mrefu, uwezo wake wa internet ni ya kasi zaidi, Pia uwezo wake wa kupiga picha ni wa kiwango cha hali ya juu zaidi.
Pia tunatoa warranty yake ambayo ni mwaka mmoja na miezi mitatu, kwa kufanya hivyo utamfanya mteja anayesoma tangazo hilo avutike na biashara unayouza/ kuifanya.
Kitendo cha kusema nauza simu fulani kwa maelezo zaidi wasiliana nami ni sawa na kumwambia mteja asije hii ni kwa sababu utakuwa hujamvutia kwa kitu chochote
Kila wakati mteja huwa ananua bidhaa fulani ili kuweza kutatua matatizo au changamoto zinazomkabili hivyo ukiweza kumteka mteja kwa kumpa suluhisho la tatizo ambalo linamkuba utamfanya mteja huyo afutiwe na wewe mwisho atakuwa umemfanya kuwa mteja wako.